Yesu Awalisha Watu Elfu Tano

30 Wale wanafunzi kumi na wawili waliporudi, walimweleza Yesu mambo yote waliyofanya na kufundisha. 31 Kwa kuwa watu wengi mno walikuwa wakija na kutoka, hata wakakosa nafasi ya kula, Yesu aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni peke yetu mahali pa faragha, mpate kupumzika.” 32 Basi wakaondoka kwa mashua peke yao wakaenda mahali pasipo na watu.

33 Lakini watu waliowaona wakiondoka, wakawatambua. Wakawa tangulia mbio kwa miguu kutoka miji yote wakielekea kule waliko kuwa wakienda. Wakawahi kufika.

34 Yesu alipofika nchi kavu na kuuona huo umati wa watu, aliwaonea huruma kwa maana walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Kwa hiyo akaanza kuwafundisha mambo mengi.

35 Hata saa za mchana zilipoanza kupita, wanafunzi wake wakamwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa zimek wenda. 36 Waruhusu watu waondoke wakajinunulie chakula kwenye mashamba na vijiji vya jirani.”

37 Lakini Yesu akawajibu, “Wapeni ninyi chakula.” Wakam wambia, “Tunahitaji fedha nyingi sana, kununulia mikate ya kutosha kulisha watu wote hawa.”

38 Akawauliza, “Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Waliporudi wakamwambia, “Ipo mikate mitano na samaki wawili.”

39 Kisha Yesu akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye nyasi, 40 nao wakaketi kwenye makundi ya watu mia mia na hamsini hamsini. 41 Yesu akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili akatazama mbinguni, akashukuru, kisha akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake wawagawie wale watu. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. 42 Watu wote wakala, wakashiba. 43 Wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia wakajaza vikapu kumi na viwili. 44 Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.

Read full chapter