Yesu Amponya Mtu Aliyelemaa Mkono

Yesu aliingia tena katika sinagogi na mtu mmoja aliyelemaa mkono alikuwapo pia. Baadhi ya watu waliokuwa wakimtega, ili wapate sababu ya kumshtaki, walimtazama kwa makini waone kama atamponya huyo kilema siku ya sabato. Yesu akamwambia yule mwe nye mkono uliolemaa, “Njoo hapa mbele.”

Yesu akawauliza, “Ni lipi lililo halali siku ya sabato? Kufanya jema, au baya? Kusalimisha maisha au kuua?” Wakakaa kimya.

Yesu akawatazama kwa hasira, akahuzunishwa na ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akauny oosha, nao ukapona kabisa! Kisha Mafarisayo wakatoka nje, wakaenda kushauriana na kundi la wafuasi wa Herode mbinu za kum wua Yesu.

Read full chapter