21 “Hakuna mtu anayeshonea kiraka cha nguo mpya kwenye nguo iliyochakaa. Akifanya hivyo, ile nguo iliyochakaa itachanika zaidi pale penye kiraka kipya na kuharibika zaidi. 22 Wala hakuna mtu anayeweka divai mpya katika viriba vya zamani. Akifa nya hivyo, ile divai mpya itavipasua hivyo viriba, kwa hiyo ata poteza divai na viriba pia. Divai mpya huwekwa kwenye viriba vipya.”

Yesu Afundisha Kuhusu Sabato

23 Siku moja ya sabato, Yesu pamoja na wanafunzi wake, wal ikuwa wakipita katikati ya mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakaanza kuvunja masuke ya ngano. 24 Mafarisayo wakamwambia, “Mbona wanafanya jambo ambalo si halali kufanywa siku ya sabato?”

25 Yesu akawaambia, “Hamjasoma alivyofanya Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? 26 Aliingia katika nyumba ya Mungu wakati Abiatha akiwa kuhani mkuu, akala mkate wa sadaka walioruhusiwa kuula ni makuhani peke yao - na akawagawia wafuasi wake.” 27 Kisha akawaambia, “Sabato iliwekwa kwa faida ya mwanadamu, lakini mwanadamu hakuwekwa kwa ajili ya sabato. 28 Na mimi, Mwana wa Adamu, ni Bwana hata wa sabato.”

Read full chapter