Mpango Wa Kumwua Yesu

14 Siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na sherehe ya mikate isiyotiwa chachu, makuhani wakuu na walimu wa sheria wali kuwa wakitafuta njia ya kumkamata Yesu kwa siri na kumwua. Wakaambiana, “Jambo hili tusilifanye wakati wa sikukuu maana watu wanaweza kufanya ghasia.”

Yesu Apakwa Manukato

Yesu alikuwa Bethania nyumbani kwa Simoni ambaye aliwahi kuwa na ukoma. Alipokuwa mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia ndani akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akammiminia Yesu manukato hayo kichwani. Baadhi ya watu waliokuwapo wali chukia wakasema, “Kwa nini anapoteza bure manukato hayo? Si afadhali yangeliuzwa kwa dinari zaidi ya mia tatu na fedha hizo wakapewa maskini?” Wakamkemea huyo mama kwa hasira. Lakini Yesu akawaambia, “Kwa nini mnamnyanyasa? Mwacheni! Amenitendea jambo zuri na jema. Maskini mnao wakati wote na mnaweza kuwapa tia msaada wakati wo wote mtakapo. Lakini hamtakuwa nami wakati wote. Huyu mama amenitendea lile aliloweza. Amenipaka manukato kuniandaa kwa mazishi yangu. Nawaambieni hakika, mahali po pote duniani ambapo Habari Njema itahubiriwa, jambo hili alilo nitendea huyu mama, litatajwa kwa ukumbusho wake.”

Yuda Anapanga Kumsaliti Yesu

10 Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa makuhani wakuu kuwaambia kuwa yuko tayari kuwasaidia wamkamate Yesu. 11 Walifurahishwa sana na habari hizi, wakaahidi kumlipa fedha. Kwa hiyo yeye akaanza kutafuta nafasi nzuri ya kumsaliti.

Yesu Anakula Pasaka Na Wanafunzi Wake

12 Siku ya kwanza ya sherehe ya Mikate isiyotiwa chachu siku ambayo kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wake walimwuliza Yesu, “Unapenda tukuandalie wapi chakula cha Pasaka?” 13 Aka watuma wanafunzi wawili akawaagiza, “Nendeni mjini. Huko mtaku tana na mwanamume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni, 14 na pale atakapoingia, mwambieni mwenye nyumba, ‘Mwalimu anasema hivi, kiko wapi chumba ambamo nitakula Pasaka pamoja na wanafunzi wangu?’ 15 Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani kilichopangwa tayari. Tuandalieni humo.” 16 Wale wanafunzi walikwenda mjini wakakuta kila kitu kama alivyowaambia; wakaandaa chakula cha Pasaka. 17 Ilipofika jioni, Yesu akaja pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 18 Walipokuwa mezani wakila, akawaambia, “Ninawaam bia hakika, mmoja wenu anayekula pamoja nami, atanisaliti.” 19 Wote wakasikitika. Wakamwuliza mmoja mmoja, “Ni mimi, Bwana?” 20 Akawajibu, “Ni mmoja wenu kumi na wawili, yule anayechovya kipande chake cha mkate kwenye bakuli pamoja nami. 21 Mimi Mwana wa Adamu sina budi kufa kama maandiko yasemavyo. Lakini ole wake yeye atakayenisaliti. Ingelikuwa heri kama hakuz aliwa!”

Chakula Cha Bwana

22 Walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akashukuru , akaumega akawapa wanafunzi wake akisema, “Pokeeni, huu ni mwili wangu.” 23 Kisha akachukua kikombe, akashukuru, akawapa, wote wakanywa humo. 24 Akawaambia, “Hii ni damu yangu ya agano, inayomwagwa kwa faida ya wengi. 25 Nawaambieni hakika, sita kunywa tena divai mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya katika Ufalme wa Mungu.”

26 Walipokwisha kuimba wimbo walikwenda kwenye mlima wa

Yesu Atabiri Kuwa Petro Atamkana

28 Yesu akawaambia, “Ninyi nyote mtakimbia mniache kwa maana imeandikwa: ‘Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika.’ 29 Lakini nikisha fufuka nitawatangulia kwenda Galilaya. 30 Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.” Yesu akamwambia, “Ninakwambia hakika, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakanusha mara tatu kwamba hunifahamu.” 31 Lakini Petro akasisitiza, “Hata kama ni lazima niuawe pamoja nawe, sitakukana.” Na wale wanafunzi wen gine wote wakasema hivyo hivyo.

Yesu Anasali Bustanini Gethsemane

32 Wakafika mahali paitwapo Gethsemane, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati mimi naomba.” 33 Kisha aka wachukua Petro na Yakobo na Yohana. Akawa na huzuni na uchungu mwingi. 34 Akawaambia, “Moyo wangu umejaa huzuni kiasi cha kufa; kaeni hapa mkeshe.” 35 Akaenda mbele kidogo, akajitupa chi ni akaomba kuwa kama ikiwezekana saa hiyo ya mateso aiepuke. 36 Akasema, “Aba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Tafadhali niondolee kikombe hiki cha mateso. Lakini si kama nitakavyo mimi, bali mapenzi yako yatimizwe.” 37 Akarudi, akakuta wame lala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Hukuweza kukesha hata kwa saa moja? 38 Kesheni na kuomba msije mkaingia katika majar ibu. Roho i radhi lakini mwili ni dhaifu.” 39 Akaondoka tena akaenda kuomba akisema maneno yale yale. 40 Aliporudi tena ali wakuta wanafunzi wake wamelala; macho yao yalikuwa mazito na hawakujua la kumwambia. 41 Aliporudi mara ya tatu aliwaambia, “ Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imefika. Mimi Mwana wa Adamu ninatiwa mikononi mwa wenye dhambi. 42 Amkeni twendeni, tazameni, yule ambaye amenisaliti amekaribia.”

Yesu Akamatwa

43 Yesu alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akafika pamoja na umati wa watu wenye mapanga na marungu. Watu hao walikuwa wametumwa na makuhani wakuu, waandishi, na wazee. 44 Yuda, yule msaliti, alikuwa amewapa ishara wale watu kuwa, “Yule nitakayembusu, ndiye mnayemtaka, mkamateni na kumchukua akiwa chini ya ulinzi.”

45 Kwa hiyo Yuda alipofika, alimwendea Yesu akamwambia, “Mwalimu,” akambusu. 46 Wakamkamata Yesu, wakamweka chini ya ulinzi. 47 Lakini mmoja wa wale waliokuwa wamesimama hapo aka chukua upanga akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio. 48 Kisha Yesu akasema, “Mbona mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu? Kwani mimi ni jambazi? 49 Siku zote nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni wala hamkunikamata. Lakini Maandiko lazima yatimie. ” 50 Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia. 51 Kijana mmoja aliyekuwa amevaa shuka tu alikuwa akimfuata Yesu. Walipomkamata, 52 alikimbia uchi, akaacha shuka lake.

Yesu Afikishwa Barazani

53 Kisha wakampeleka Yesu nyumbani kwa kuhani mkuu ambapo makuhani wakuu, wazee, na walimu wa sheria walikuwa wamekuta nika. 54 Petro aliwafuata kwa mbali, akaingia barazani kwa kuhani mkuu, akaketi pamoja na walinzi akiota moto. 55 Makuhani wakuu na wajumbe wote wa Baraza walijaribu kutafuta ushahidi wa kumshtaki Yesu ili wapate kumwua, lakini hawakupata. 56 Wengi walitoa ushahidi wa uongo, lakini ushahidi wao haukupatana.

57 Ndipo watu fulani wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo wakisema, 58 “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitabomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga lin gine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ” 59 Lakini hata hawa, ushahidi wao ulipingana.

60 Kuhani Mkuu akasimama mbele ya Baraza akamwuliza Yesu, “Huwezi kujibu mashtaka haya ambayo watu hawa wameleta juu yako?” 61 Lakini Yesu alikaa kimya; hakusema neno lo lote. Kuhani Mkuu akamwuliza, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu Mtu kufu?” 62 Yesu akajibu, “Mimi ndiye, na mtaniona mimi Mwana wa Adamu nimeketi upande wa kulia wa Mungu Mwenyezi, na nikija na mawingu ya mbinguni.”

63 Kuhani Mkuu akararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi? 64 Ninyi wote mmemsikia akikufuru! Mna toa hukumu gani?” Wote wakamhukumu kwamba ana hatia na auawe.

65 Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa usoni wakampiga na kumwambia, “Toa unabii, utuambie nani amekupiga!” Maaskari wakampokea kwa mapigo.

Petro Amkana Yesu

66 Petro alikuwa bado yuko barazani. Kisha akaja mtumishi mmoja wa kike wa kuhani mkuu. 67 Alipomwona Petro akiota moto, alimtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu Mnazareti.” 68 Lakini Petro akakataa, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema,” akaondoka akaenda mlangoni. 69 Yule mtumi shi wa kike akamwona, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama pale, “Huyu mtu ni mmoja wao.” 70 Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo pamoja naye wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!” 71 Petro akaanza kulaani na kuapa, akawaambia, “Simjui huyo mtu mnayemsema.”

72 Hapo hapo jogoo akawika mara ya pili. Petro akakumbuka lile neno ambalo Yesu alikuwa amemwambia, “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akalia kwa uchungu. Pilato Anamhoji Yesu

15 Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya mkutano pamoja na wazee na walimu wa sheria, na Baraza zima likafanya mashauri. Wakamfunga Yesu, wakamchukua na kumkabidhi kwa Pilato. Pilato akamwuliza, “Wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe ndiye uliyesema maneno hayo.” Makuhani wakuu wakamsh taki kwa mambo mengi. Pilato akamwuliza tena, “Huna la kujibu?

Unasikia mashtaka yao!”

Yesu hakusema neno. Pilato akashangaa.

Yesu Ahukumiwa Kifo

Ilikuwa desturi wakati wa sherehe za Pasaka kumfungulia mfungwa ye yote ambaye watu walimtaka . Wakati huo, mtu mmoja aitwaye Baraba alikuwa amefungwa gerezani pamoja na wahalifu wen gine kwa makosa ya kusababisha uasi ambapo mauaji yalitokea. Basi watu waliokusanyika walimjia Pilato wakamwomba awafanyie kama ilivyokuwa desturi wakati wa Pasaka. Pilato akawauliza, “Mnataka nimfungue huyu mfalme wa Wayahudi?” 10 Alikuwa ana fahamu kwamba wakuu wa makuhani walikuwa wanamwonea Yesu wivu ndio sababu wakamshtaki kwake. 11 Lakini makuhani wakuu wakawa chochea watu wamwombe awafungulie Baraba.

12 Pilato akawauliza tena watu, “Nimfanye nini huyu mtu mnayemwita mfalme wa Wayahudi?” 13 Wakapiga kelele, “Msulub ishe!” 14 Akawauliza, “Kwa nini? Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakapiga kelele kwa nguvu zaidi, “Msulubishe!”

15 Pilato alitaka kuwaridhisha watu, kwa hiyo akamfungulia Baraba; na baada ya kuamuru Yesu apigwe mijeledi, akamtoa asulub ishwe.

Maaskari Wamdhihaki Yesu

16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. 18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.

Yesu Asulubishwa

21 Walipokuwa wakienda kumsulubisha, njiani walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, raia wa Kirene. Yeye alikuwa baba yao Aleksanda na Rufas. Alikuwa anakuja mjini kutoka shamba. Wakamla zimisha abebe msalaba wa Yesu. 22 Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgota, -yaani Mahali pa Fuvu la Kichwa.

23 Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini akaikataa. 24 Basi wakamsulubisha, wakagawana nguo zake kwa kuzipigia kura kuamua kila mtu achukue nini.

25 Ilikuwa yapata saa tatu asubuhi walipomsulubisha. 26 Tangazo la mashtaka yake liliandikwa maneno haya: “MFALME WA WAYAHUDI.” 27 Majambazi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wa kushoto. [ 28 Na kwa njia hii yale Maandiko yasemayo, “Alihesabiwa pamoja na wenye hatia,” yalitimia.] 29 Watu waliokuwa wakipita, walimtukana na kutikisa vichwa vyao kwa mzaha wakasema, “Si ulikuwa ukisema kwamba unaweza kulivunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu? 30 Shuka msalabani basi, ujiokoe mwenyewe!” 31 Hali kadhalika makuhani wakuu na walimu wa sheria walimdhihaki wakisema, “Ali waokoa wengine lakini anashindwa kujiokoa mwenyewe. 32 Kristo mfalme wa Wayahudi ashuke basi msalabani ili tupate kuona na kuamini!” Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia walimtukana.

Kifo Cha Yesu Msalabani

33 Ilipofika saa sita, giza lilikumba nchi nzima kwa muda wa saa tatu. 34 Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu “Eloi, Eloi lama Sabaktani?” Yaani, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” 35 Baadhi ya watu waliokuwa wanasimama karibu waliposikia maneno hayo, walisema, “Mnamsikia? Anamwita

Eliya!”

36 Mtu mmoja akaenda mbio, akachovya sponji kwenye divai na siki, akaiweka kwenye ufito akamwinulia Yesu ili anywe huku akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumshusha kutoka msala bani!”

37 Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. 38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili kuanzia juu hadi chini.

39 Yule askari aliyekuwa amesimama mbele ya msalaba alipoona jinsi alivyokata roho, akasema, “Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

40 Walikuwapo pia wanawake walio kuwa wakiangalia mambo haya kwa mbali. Kati yao walikuwapo Mariamu Magdalena, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na pia Salome . 41 Hawa walifuatana na Yesu alipokuwa Galilaya na kumhudumia. Pia walikuwapo wanawake wengine wengi waliokuwa wamekuja naye Yerusalemu.

Mazishi Ya Yesu

42 Ilipofika jioni, kwa kuwa ilikuwa siku ya Maandalizi, siku moja kabla ya Pasaka, 43 Yusufu wa Arimathea alijikaza akamwendea Pilato akamwomba auchukue mwili wa Yesu. Yeye alikuwa ni mjumbe wa Baraza aliyeheshimika, ambaye alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. 44 Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu amekwisha kufa. Kwa hiyo akamwita askari amhakikishie kuwa kweli amekufa. 45 Baada ya kuhakikishiwa na yule askari kwamba kweli amekufa, Pilato alimpa Yusufu ruhusa ya kuuchukua mwili wa Yesu. 46 Basi Yusufu alinunua sanda ya kitani, akautoa mwili wa Yesu msalabani; akamzungushia sanda, akamweka ndani ya kaburi lililochongwa kwenye mwamba. Kisha akaviringisha jiwe akaufunika mlango wa kaburi. 47 Mariamu Magdalena na Mariamu mama wa Yose walipaona mahali alipozikwa Yesu.