34 Ni kama mtu anayesafiri na kuwaachia wat umishi wake madaraka, kila mtu na wajibu wake; kisha akamwambia mlinzi wa mlango awe macho. 35 Kesheni basi, kwa sababu hamjui ni lini bwana mwenye nyumba atarudi. Anaweza akaja jioni, au usiku wa manane au alfajiri au mapambazuko. 36 Kama akija gha fla, pasipo ninyi kumtazamia, asije awakute mmelala. 37 Na haya ninayowaambia ninyi nawaambia watu wote: Kesheni!”

Read full chapter