Kuhusu Ufufuo wa Wafu

18 Kisha Masadukayo, ambao wanaamini kuwa hakuna ufufuo wa wafu, walimjia Yesu wakamwuliza swali wakisema, 19 “Mwalimu, Musa alituandikia agizo kuwa kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi ndugu yake hana budi kumwoa mjane huyo ili amzalie ndugu yake watoto. 20 Sasa walikuwapo ndugu saba. Yule wa kwanza akaoa akafariki pasipo kupata mtoto. 21 Wapili akam woa yule mjane, naye akafariki bila kuacha mtoto. Ikawa hivyo hata kwa yule wa tatu. 22 Kwa kifupi, ndugu wote saba walimwoa huyo mjane lakini wote hawakuzaa naye. Hatimaye yule mama naye akafariki. 23 Sasa tuambie, wakati wa ufufuo, watakapofufuka wote, huyo mama aliyeolewa na ndugu wote saba, atakuwa mke wa nani?”

24 Yesu akawajibu, “Mmekosea kabisa kwa maana hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu.” 25 Wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni . 26 Na kuhusu ufufuo wa wafu: hamjasoma katika kitabu cha Musa, sehemu ile inayoelezea jinsi Mungu alivyozungumza na Musa kutoka katika kichaka akisema, ‘Mimi, ni Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo’? 27 Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai. Kwa hiyo mmekosea kabisa.”

Read full chapter