Mfano Wa Shamba La Mizabibu Na Wakulima Waovu

12 Yesu alianza kusema nao kwa kutumia mifano: “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu; akalizungushia uzio, akachimba kisima cha kutengenezea divai na akajenga mnara. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima fulani kisha akasafiri kwenda nchi nyingine. Wakati wa mavuno ulipofika, mwenye shamba alimtuma mtumishi wake kwa hao wakulima kuchukua sehemu yake ya mavuno. Lakini wale wakulima walimkamata yule mtumishi, wakampiga, wakamfukuza mikono mitupu. Yule mwenye shamba akamtuma mtum ishi mwingine. Wale wakulima wakampiga kichwani, na kumfanyia mambo ya aibu. Akapeleka mtumishi mwingine tena. Huyu, wakam wua. Akapeleka wengine zaidi, baadhi yao wakawapiga na wengine wakawaua. Mwenye shamba akawa amebakiwa na mtu mmoja tu ambaye angeweza kumtuma. Huyu alikuwa mwanae aliyempenda sana. Hatimaye akaamua kumtuma akisema, ‘Bila shaka watamheshimu mwanangu.’ Lakini wale wakulima wakashauriana, ‘Huyu mwanae ndiye mrithi. Tumwue na urithi utakuwa wetu.’ Wakamchukua, wakamwua, wakam tupa nje ya shamba. Mnadhani yule mwenye shamba atafanya nini? Atakuja, awaue hao wakulima kisha alikodishe shamba lake kwa wak ulima wengine.

Read full chapter