Amri Iliyo Kuu

28 Mwalimu mmoja wa sheria aliwasikiliza wakijadiliana. Alipoona kwamba Yesu amewajibu vizuri, naye akamwuliza, “Katika amri zote, ni ipi iliyo kuu?” 29 Yesu akamjibu, “Iliyo kuu ni hii, ‘Sikiliza Israeli, Bwana Mungu wetu ndiye Bwana pekee. 30 Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote.’ 31 Na sheria ya pili kwa ukuu ndio hii: ‘Mpende jirani yako kama nafsi yako.’ Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.”

32 Yule mwalimu wa sheria akamwambia Yesu, “Mwalimu, ume jibu vyema. Ulivyosema ni kweli kabisa, Mungu ni mmoja wala hakuna mwingine ila yeye. 33 Na kumpenda Mungu kwa moyo wote na kwa akili zote na kwa nguvu zote; na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda ni bora zaidi kuliko kutoa sadaka ya kuteketezwa.”

34 Yesu alipoona jinsi alivyojibu kwa busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Tangu wakati huo, hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali zaidi.

Read full chapter

Amri ipi ni ya Muhimu Zaidi?

(Mt 22:34-40; Lk 10:25-28)

28 Mwalimu wa Sheria alifika naye aliwasikia wakijadiliana. Alipoona jinsi Yesu alivyowajibu vizuri sana, alimwuliza, “Je, amri ipi ni muhimu sana kuliko zote?”

29 Yesu akajibu, “Muhimu sana ni hii: ‘Sikiliza, Israeli, Bwana Mungu wetu ni mmoja. 30 Nawe unapaswa kumpenda Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa nafsi yako yote, na kwa akili zako zote, na kwa nguvu zako zote.’(A) 31 Amri ya pili ni hii: ‘mpende jirani yako[a] kama unavyojipenda mwenyewe.’(B) Hakuna amri nyingine kubwa kuliko hizi.”

32 Na mwalimu wa Sheria akamwambia, “Umejibu vema kabisa mwalimu. Upo sahihi kusema kuwa Mungu ni mmoja, na hakuna mwingine ila yeye. 33 Ni muhimu zaidi kumpenda Mungu kwa moyo wako wote, kwa ufahamu wako wote, na kwa nguvu zako zote, na kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe kuliko sadaka zote za kuteketezwa na matoleo tunayompa Mungu.”

34 Yesu alipoona kwamba yule mtu amejibu kwa busara, alimwambia, “Wewe hauko mbali na Ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuwepo mtu mwingine aliyediriki kumwuliza maswali mengine zaidi.

Read full chapter

Footnotes

  1. 12:31 jirani yako Mafundisho ya Yesu katika Lk 10:25-37 yanaonesha kwa uwazi kuwa hii ni pamoja na yeyote mwenye uhitaji.