37 Kesho yake aliposhuka kutoka mlimani alikutana na umati mkubwa wa watu. 38 Ghafla, mtu mmoja kati yao akapiga kelele akasema, “Mwalimu, tafadhali nakuomba umwangalie mtoto wangu, ni mwanangu wa pekee. 39 Mara kwa mara pepo humshika na kumfanya apige kelele kisha humwangusha na kumtia kifafa akatokwa na povu mdomoni. Anamtesa sana na hamwachii ila kwa shida. 40 Nimewaomba wanafunzi wako wamwondoe huyo pepo lakini wameshindwa.” 41 Yesu akajibu, “Enyi watu mliopotoka, msio na imani, nitakaa nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”

42 Yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo akamwangusha, akam tia kifafa. Lakini Yesu akamwamuru yule pepo amtoke. Akamponya yule mtoto akamkabidhi kwa baba yake. 43 Watu wote walishangaa walipoona huo uweza mkuu wa Mungu. Wakati watu walipokuwa wanas taajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Yesu, yeye aliwaambia wanafunzi wake: 44 “ Sikilizeni kwa makini haya nitakayowaambia sasa: mimi Mwana wa Adamu nitasalitiwa na kuwekwa mikononi mwa wanadamu.” 45 Lakini wanafunzi wake hawakuyaelewa maneno hayo. Maana ya maneno hayo ilikuwa imefichwa ili wasiweze kuelewa, nao waliogopa kumwuliza.

Yesu Afundisha Kuhusu Ukubwa

46 Wanafunzi wakaanza kubishana wao kwa wao kuhusu nani kati yao alikuwa mkuu zaidi. 47 Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao, akamsimamisha mtoto mdogo karibu naye 48 kisha akawaambia, “Ye yote atakayemkaribisha mtoto huyu mdogo kwa jina langu atakuwa amenikaribisha; na ye yote atakayenikaribisha mimi atakuwa amem karibisha yeye aliyenituma; kwa maana yeye aliye mdogo kati yenu, ndiye aliye mkubwa kuliko wote.” 49 Yohana akasema, “Bwana, tumemwona mtu akifukuza pepo kwa jina lako tukamzuia kwa maana yeye si mmoja wetu.”

Read full chapter