Bwana Wa Sabato

Siku moja ya sabato Yesu alikuwa akipita katika mashamba ya ngano. Wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke ya ngano, wakayafi kicha na kula punje zake. Baadhi ya Mafarisayo wakawauliza, “Mbona mnavunja sheria kwa kuvuna ngano siku ya sabato?”

Yesu akawajibu, “Ninyi hamsomi Maandiko? Hamjasoma alicho fanya Mfalme Daudi wakati yeye na wafuasi wake walipokuwa na njaa? Aliingia Hekaluni, akachukua ile mikate ya madhabahuni -ambayo huliwa na makuhani peke yao -akala, kisha akawapa na wafuasi wake wakala!” Akaongezea kusema, “Mimi Mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato.”

Read full chapter