37 Wala watu hawaweki divai mpya katika viriba vilivyochakaa; ukifanya hivyo, hivyo viriba vitapa suka na divai yote itamwagika. 38 Divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya. 39 Na pia hakuna mtu anayependelea divai mpya baada ya kunywa divai iliyoiva vizuri. Kwa maana husema, ‘Hii divai iliyoiva siku nyingi ni bora zaidi.’ ”

Read full chapter

37 Pia hakuna mtu anayeweka divai mpya[a] katika viriba vya zamani. Divai mpya itavipasua, divai itamwagika, na viriba vitaharibika. 38 Daima mnaweka divai mpya kwenye viriba vipya. 39 Hakuna mtu ambaye baada ya kunywa divai ya zamani hutaka divai mpya. Kwa sababu husema, ‘Divai ya zamani ni nzuri.’”

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:37 divai mpya Maji ya zabibu ambayo ndiyo yanaanza kuchachuka na hutengeneza mgandamizo ndani ya chombo kilichofungwa.