31 Kisha akaenda Kapernaumu, mji ulioko wilaya ya Galilaya, na siku ya sabato akawafundisha watu katika sinagogi. 32 Walis taajabishwa na mafundisho yake, maana maneno yake yalikuwa na mamlaka. 33 Alikuwepo mtu mmoja katika sinagogi aliyekuwa ame pagawa na pepo mchafu, naye alianza kupiga kelele kwa nguvu akisema, 34 “Unataka kutufanya nini, Wewe Yesu wa Nazareti? Ume kuja kutuangamiza? Nakufahamu wewe ni nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu.” 35 Yesu akamwamuru yule pepo: “Nyamaza! Mtoke!” Yule pepo akamwangusha chini yule mtu mbele yao, akamtoka pasipo kumd huru. 36 Watu wote wakashangaa wakaambiana, “Mafundisho ya mtu huyu ni ya ajabu. Anawaamuru pepo wachafu kwa mamlaka na nguvu, nao wanatoka! 37 Habari zake zikaenea pote katika mkoa ule.

Yesu Awaponya Wengi

38 Alipotoka katika sinagogi Yesu alikwenda nyumbani kwa Simoni na alipofika huko alimkuta mama mkwe wa Simoni ana homa kali. Wakamwomba sana amponye. 39 Basi Yesu akasimama kando ya kitanda chake akaiamuru ile homa imtoke. Homa ikamtoka yule mama. Akaamka mara moja akaanza kuwahudumia. 40 Jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwa Yesu. Akamgusa kila mgonjwa, akawaponya wote. 41 Pepo wachafu pia waliwatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walifahamu kuwa yeye ni Kristo.

42 Kesho yake, kulipopambazuka, Yesu alikwenda mahali pa faragha. Watu wengi wakawa wanamtafuta kila mahali, na walipom wona wakajaribu kumzuia asiondoke. 43 Lakini yeye akawaambia, “Ninao wajibu wa kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu sehemu nyingine pia. Hii ndio sababu nilitumwa.”

Read full chapter