39 Mmoja kati ya wale wahalifu waliosulubiwa naye akamtu kana, akasema: “Wewe si ndiye Kristo? Jiokoe na utuokoe na sisi.”

40 Yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake, akisema, “Wewe humwogopi hata Mungu! Wote tumehukumiwa adhabu sawa. 41 Adhabu yetu ni ya haki kwa sababu tunaadhibiwa kwa makosa tuliyofanya. Lakini huyu hakufanya kosa lo lote.” 42 Kisha akasema, “Bwana Yesu unikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.” 43 Yesu akam jibu, “Nakuambia kweli, leo hii utakuwa pamoja nami peponi.”

Read full chapter