14 Wakati ulipofika Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. 15 Kisha akawaambia “Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. 16 Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.” 17 Akapokea kikombe cha divai akashukuru, akasema, “Chukueni mnywe wote. 18 Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.”

19 Kisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, “Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” 20 Vivyo hivyo baada ya kula, aka chukua kile kikombe cha divai akasema, “Hiki kikombe ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.

Read full chapter