27 Baadhi ya Masadukayo , wale wanaosema kwamba hakuna ufu fuo wa wafu, wakamjia Yesu wakamwuliza, 28 “Mwalimu, katika sheria ya Musa , tunasoma kwamba kama mtu akifariki akamwacha mkewe bila mtoto, basi kaka yake amwoe huyo mjane ili amzalie marehemu watoto. 29 Walikuwepo ndugu saba. Wa kwanza akafa bila kuzaa mtoto. 30 Kaka wa pili akamwoa huyo mjane 31 na wa tatu pia. Ikawa hivyo mpaka ndugu wote saba wakawa wamemwoa huyo mama na wote wakafa pasipo kupata mtoto. 32 Mwishowe mama huyo naye akafa. 33 Je, siku ya ufufuo, mwanamke huyo ambaye aliolewa na wote saba atahesabiwa kuwa ni mke wa nani?”

34 Yesu akawajibu , “Katika maisha haya watu huoa na kuol ewa, 35 lakini wale ambao Mungu atawaona wanastahili kufufuka kutoka kwa wafu, watakapofika mbinguni hawataoa au kuolewa. 36 Hawa hawawezi kufa tena kwa sababu wao ni kama malaika; wao ni wana wa Mungu kwa kuwa wamefufuka kutoka kwa wafu. 37 Hata Musa alidhihirisha kuwa wafu wanafufuka. Alimwita Bwana, ‘Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo,’ wakati Mungu aliposema naye katika kile kichaka kilichokuwa kikiwaka bila kuungua. 38 Yeye ni Mungu wa watu walio hai na si Mungu wa wafu kwa sababu kwa Mungu watu wote ni hai.” 39 Baadhi ya walimu wa sheria wakasema, “Mwalimu, umesema sawa kabisa!” 40 Na hakuna mtu aliyethubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.

Read full chapter