42 akasema kwa sauti kubwa: “Umebarikiwa wewe zaidi ya wanawake wengine wote, naye mtoto utakayemzaa amebari kiwa. 43 Sikustahili heshima hii ya kutembelewa na mama wa Bwana wangu! 44 Mara tu niliposikia salaamu zako, mtoto aliyeko tum boni mwangu aliruka kwa furaha. 45 Wewe umebarikiwa kwa kuwa uliamini kwamba Bwana atatimiza yale aliyokuambia.”

Read full chapter