47 Kila siku alikuwa akifundisha Hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa sheria wakiungwa mkono na viongozi wengine walijaribu kila njia wapate kumwua 48 lakini hawakupata nafasi kwa sababu watu wote waliomfuata waliyasikiliza maneno yake kwa makini na kuyazingatia. Yesu Aulizwa Kuhusu Mamlaka Yake

20 Siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu Hekaluni na kuhubiri habari njema, wakuu wa makuhani, walimu wa sheria na wazee walifika Hekaluni