12 Kwa hiyo akawaambia: “Mtu mmoja wa ukoo wa kitawala, alisafiri kwenda nchi ya mbali ili akapokee madaraka ya kuwa mfalme, kisha arudi. 13 Akawaita watumishi wake kumi akawapa kila mmoja fungu la fedha. Akawaambia, ‘Zitumieni kufanyia biash ara mpaka nitakaporudi.’ 14 Lakini raia wake walimchukia wakapeleka ujumbe usemao, ‘Hatutaki huyu mtu awe mfalme wetu. ’ 15 Hata hivyo alipewa ufalme akarudi nyumbani. Kisha akawaita wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha, ili afahamu faida kila mmoja wao aliyopata.

16 “Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, kutokana na fedha uliyoniachia nimepata faida mara kumi zaidi.’ 17 Yule bwana akamjibu, ‘Umefanya vizuri mtumishi mwema! Kwa sababu umekuwa mwaminifu katika wajibu mdogo sana, nakupa mamlaka juu ya miji kumi.’

18 “Wa pili naye akaja, akasema, ‘Bwana, fedha yako imeleta faida mara tano zaidi.’ 19 Bwana wake akajibu, ‘Nakupa mamlaka juu ya miji mitano.’ 20 Kisha akaja mtumishi mwingine akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako. Niliitunza vizuri kwenye kitambaa. 21 Nilikuogopa, kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unachukua ambapo hukuweka kitu na unavuna mahali ambapo hukupanda kitu.’

22 “Bwana wake akamjibu, ‘Nitakuhukumu kwa maneno yako mwe nyewe, wewe mtumishi mwovu ! Kama ulifahamu kwamba mimi ni mtu mkali, nichukuaye mahali ambapo sikuweka kitu na kuvuna ambapo sikupanda; 23 kwa nini basi hukuweka fedha zangu benki ili nita kaporudi nizichukue na faida yake?’ 24 Ndipo akawaambia wale waliokuwa wamesimama karibu , ‘Mnyang’anyeni fungu lake la fedha mkampe yule mwenye kumi.’ 25 Wakamwambia, ‘Bwana, mbona tayari anayo mafungu kumi’? 26 Akajibu, ‘Nawahakikishieni kwamba, kila aliye na kitu, Mungu atamwongezea; na yule asiyetumia alicho nacho, atanyang’anywa hata hicho alicho nacho. 27 Sasa nileteeni wale maadui zangu ambao hawakutaka mimi niwe mfalme wao; waleteni hapa muwaue mbele yangu.”’

Read full chapter