10 Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 yule Farisayo alisimama akasali kimoyomoyo. ‘Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine: wany ang’anyi, wadhalimu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma na kutoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali. Hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto akasema, ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.”

Read full chapter

10 “Siku moja Farisayo na mtoza ushuru walikwenda Hekaluni kuomba. 11 Farisayo alisimama peke yake mbali na mtoza ushuru. Farisayo aliomba akisema, ‘Ee Mungu, ninakushukuru kwa kuwa mimi si mwovu kama watu wengine. Mimi siyo kama wezi, waongo au wazinzi. Ninakushukuru kwa kuwa mimi ni bora kuliko huyu mtoza ushuru. 12 Ninafunga mara mbili kwa wiki na kutoa sehemu ya kumi ya vyote ninavyopata!’

13 Mtoza ushuru alisimama peke yake pia. Lakini alipoanza kuomba, hakuthubutu hata kutazama juu mbinguni. Alijipigapiga kifua chake akijinyenyekeza mbele za Mungu. Akasema, ‘Ee Mungu, unihurumie, mimi ni mwenye dhambi.’ 14 Ninawaambia, mtu huyu alipomaliza kuomba na kwenda nyumbani, alikuwa amepatana na Mungu. Lakini Farisayo, aliyejisikia kuwa bora kuliko wengine, hakuwa amepatana na Mungu. Watu wanaojikweza watashushwa. Lakini wale wanaojishusha watakwezwa.”

Read full chapter