Shilingi Iliyopotea

“Au tuseme mwanamke ana shilingi kumi halafu apoteze moja. Si atawasha taa afagie nyumba na kutafuta kwa uangalifu mpaka aipate? Na akisha kuipata atawaita marafiki zake na majirani na kuwaambia, ‘Furahini pamoja nami; nimeipata ile shilingi yangu iliyopotea!’

Read full chapter

Fikiria kuhusu mwanamke mwenye sarafu kumi za fedha,[a] lakini akapoteza sarafu moja kati ya hizo. Atawasha taa na kuifagia nyumba. Ataitafuta sarafu kwa bidii mpaka aione. Na akiiona, atawaita rafiki na jirani zake na kuwaaambia, ‘Furahini pamoja nami, kwa sababu nimeipata sarafu niliyoipoteza!’

Read full chapter

Footnotes

  1. 15:8 sarafu kumi za fedha Kila sarafu, Sarafu ya Kiyunani iliyoitwa drachma ilikuwa na thamani ya ujira au mshahara wa siku moja.