16 Yesu akamjibu, ‘ ‘Mtu mmoja alikuwa anaandaa karamu kubwa, akaalika watu wengi. 17 Wakati wa sherehe ulipofika, akamtuma mtumishi wake akawaam bie walioalikwa, ‘Karibuni, kila kitu ni tayari sasa.’ 18 Lakini wote, mmoja mmoja, wakaanza kutoa udhuru. Wa kwanza akasema, ‘ Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali niwie radhi.’ 19 Mwingine akasema, ‘Nimenunua ng’ombe wa kulimia, jozi tano; nimo njiani kwenda kuwajaribu, tafadhali niwie radhi.’ 20 Na mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’

21 “Yule mtumishi akarudi, akampa bwana wake taarifa. Ndipo yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda upesi kwenye mitaa na vichochoro vya mjini uwalete maskini, vilema, vipofu na viwete.’

22 “Baadaye yule mtumishi akamwambia ‘Bwana, yale uliyon iagiza nimefanya, lakini bado ipo nafasi.’ 23 Ndipo yule bwana akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda kwenye barabara na njia zilizoko nje ya mji uwalazimishe watu waje mpaka nafasi zote zijae. 24 Ninawaambia, hakuna hata mmoja wa wale niliowapelekea mwaliko rasmi atakayeionja karamu yangu.”

Read full chapter