Kukesha

35 “Muwe tayari mkiwa mmevaa, na taa zenu zikiwaka. 36 Muwe kama watumishi wanaomngojea bwana wao arudi kutoka haru sini, ili atakapokuja na kugonga mlango wamfungulie mara moja. 37 Itakuwa ni heri kwa wale watumishi ambao bwana wao akija ata wakuta wanamngoja. Nawaambieni kweli, atajiandaa na kuwaketisha karamuni awahudumie. 38 Itakuwa ni furaha kubwa kwao ikiwa ata wakuta tayari hata kama atakuja usiku wa manane au alfajiri.

39 Fahamuni kwamba kama mwenye nyumba angalijua ni saa ngapi mwizi atakuja, angalijiandaa asiiachie nyumba yake ivunjwe. 40 Kwa hiyo, ninyi pia mkae tayari, kwa maana mimi Mwana wa Adamu nita kuja saa ambayo hamnitegemei.”

Mtumishi Mwaminifu Na Asiye mwaminifu

41 Ndipo Petro akamwambia, “Bwana, mfano huu unatuambia sisi peke yetu au watu wote?” 42 Yesu akamwambia, “Ni yupi wakili mwaminifu na mwenye busara? Ni yule ambaye bwana wake atamfanya mtawala juu ya nyumba yake yote naye awape watumishi wengine chakula chao wakati unaofaa. 43 Itakuwa ni furaha kwa mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 44 Ninawahakikishia kwamba atampa mamlaka juu ya vyote alivyo navyo. 45 Lakini kwa mfano, kama yule mtumishi atawaza moyoni mwake, ‘Bwana wangu anachelewa kurudi,’ halafu aanze kuwa piga wale watumishi wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa, 46 bwana wake atarudi siku ambayo hakumtazamia, na saa asiyoijua. Huyo bwana wake atamwadhibu vikali pamoja na wote wasiotii. 47 Na mtumishi ambaye anafahamu mapenzi ya bwana wake na asijiandae wala kufanya kama apendavyo bwana wake, pia ataad hibiwa vikali. 48 Lakini mtumishi ambaye hafahamu anachotakiwa kufanya na akafanya kitu kinachostahili adhabu, atapata adhabu ndogo. Mungu atatarajia vingi kutoka kwa mtu aliyepewa vipawa vingi; na mtu aliyekabidhiwa vingi zaidi, atadaiwa zaidi pia.”

Read full chapter