Font Size
Luka 11:5-8
Neno: Bibilia Takatifu
Luka 11:5-8
Neno: Bibilia Takatifu
5 Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. 6 Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ 7 Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ 8 “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica