Kisha akawaambia, “Tuseme mmoja wenu ana rafiki yake. Akamwendea usiku wa manane akamwambia, ‘Rafiki, nikopeshe mikate mitatu. Nimefikiwa na rafiki yangu akiwa safarini nami sina chakula cha kumpa.’ Yule aliyeko ndani akajibu, ‘Usinisumbue! Nimekwisha kufunga mlango. Na mimi na watoto wangu tumelala. Siwezi kuamka kukupa cho chote.’ “Nawaambieni, hata kama huyo mtu hataamka na kumpa mikate kwa sababu ni rafiki yake, lakini kwa sababu ameendelea kuomba bila kukata tamaa ataamka ampe kiasi anachohitaji.

Read full chapter