25 Mwalimu mmoja wa sheria alisimama akajaribu kumpima Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili nipate uzima wa milele?” 26 Yesu akamjibu, “Sheria inasemaje? Unaitafsiri vipi?” 27 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa nguvu zako zote na kwa akili zako zote. Na umpende jirani yako kama unavyojipenda mwe nyewe.” 28 Yesu akamwambia, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivyo nawe utaishi.” 29 Lakini yule mwalimu wa sheria akitaka kuon yesha kwamba hoja yake ilikuwa na maana zaidi, akamwuliza Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”

30 Yesu akamjibu, “Mtu mmoja aliteremka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Njiani akashambuliwa na majambazi; wakamwibia kila kitu alichokuwa nacho, wakampiga wakamwacha karibu ya kufa. 31 litokea kwamba kuhani mmoja alikuwa anapitia njia ile. Ali pomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. 32 Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.

33 “Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa akisafiri kupitia njia hiyo alipomkuta, alimwonea huruma, 34 akamwendea akasafisha maj eraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. 35 Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.

36 “Unadhani ni yupi kati ya hawa watatu alikuwa jirani yake yule mtu aliyeshambuliwa na majambazi?”

37 Yule mwalimu wa sheria akajibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akasema, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”

Read full chapter

Simulizi Kuhusu Msamaria Mwema

25 Kisha mwanasheria mmoja alisimama ili amjaribu Yesu. Akasema, “Mwalimu, ninatakiwa nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

26 Yesu akamwambia, “Imeandikwa nini katika torati? Unaielewaje?”

27 Yule mwana sheria akajibu, “‘Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote.’(A) Pia ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe.’”(B)

28 Yesu akasema, “Jibu lako ni sahihi. Fanya hivi nawe utaupata uzima wa milele.”

29 Lakini mwanasheria alitaka kuonesha kuwa alikuwa mwenye haki na aliishi kwa usahihi. Hivyo akamwuliza Yesu, “Lakini si kila mtu aliye jirani yangu, au unasemaje?”

30 Katika kujibu swali hili, Yesu akasema, “Mtu mmoja alikuwa anasafiri kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Akiwa njiani alivamiwa na majambazi, wakamchania nguo na kumpiga. Kisha wakamwacha amelala chini akiwa katika hali ya kufa.

31 Ikatokea kuwa kuhani mmoja alikuwa anasafiri kupitia njia hiyo hiyo. Alipomwona, hakusimama ili amsaidie, alikwenda zake. 32 Kisha Mlawi[a] alipokaribia na kumwona yule mtu, alipita upande mwingine. Hakusimama ili amsaidie, Alikwenda zake.

33 Ndipo Msamaria[b] mmoja aliyekuwa anasafiri kupitia njia ile ile, alipofika mahali ambapo mtu aliyejeruhiwa alikuwa amelala, alipomwona alimhurumia. 34 Alimkaribia ili amsaidie, akamsafisha majeraha kwa mafuta ya zeituni na divai,[c] kisha akayafunga majeraha yake. Msamaria alikuwa na punda. Akampandisha juu ya punda wake na kumpeleka mpaka kwenye nyumba ya wageni. Akamhudumia huko. 35 Siku iliyofuata, Msamaria alitoa sarafu mbili za fedha na kumpa mtunza nyumba ya wageni, akamwambia, ‘Mtunze mtu huyu aliyejeruhiwa. Ukitumia pesa nyingi zaidi kwa kumhudumia, nitakulipa nitakapokuja tena.’”

36 Kisha Yesu akasema, “Ni yupi kati ya hawa watu watatu unadhani hakika alikuwa jirani wa yule mtu aliyepigwa na majambazi?”

37 Mwanasheria akajibu, “Ni yule aliyemsaidia.”

Yesu akasema, “Basi nenda ukafanye kama alivyofanya.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 10:32 Mlawi Yaani mtumishi wa Hekalu.
  2. 10:33 Msamaria Wayahudi waliwachukulia Wasamaria kama maadui. Tazama Msamaria katika Orodha ya Maneno.
  3. 10:34 mafuta ya zeituni na divai Vilitumika kama dawa kwa ajili ya kulainisha na kusafisha majeraha.