Yesu Ahudhuria Sikukuu Ya Vibanda Yerusalemu

Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Aliamua kutokwenda Yudea kwa sababu Wayahudi huko wali taka kumwua. Sikukuu ya Vibanda ilipokaribia, ndugu zake Yesu walimwambia, “Ni vema utoke hapa uende Yudea ili wanafunzi wako wapate kuona miujiza unayofanya. Mtu anayetaka kujulikana, hafanyi mambo yake kwa siri. Kwa kuwa unafanya mambo haya, jion yeshe kwa ulimwengu.” Hata ndugu zake hawakumwamini.

Yesu akawajibu, “Wakati wangu wa kwenda huko haujafika. Ninyi mnaweza kwenda wakati wo wote. Ulimwengu hauwachukii ninyi lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. Ninyi nendeni kwenye sikukuu, lakini mimi sitahudhuria sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” Baada ya kusema hivyo, akabaki Galilaya.

Read full chapter