48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa. 50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51 Mimi ni mkate wa uzima uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu ataishi milele. Na mkate wenyewe ni mwili wangu ambao nitautoa ili watu wote ulimwenguni wapate kuishi milele.”

52 Hapo Wayahudi wakaanza kubishana kwa hasira wakiulizana, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”

53 Kwa hiyo Yesu akasema, “Ninawaambieni hakika, msipoula mwili wangu mimi Mwana wa Adamu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54 Mtu ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula halisi na damu yangu ni kinywaji halisi. 56 Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anaishi ndani yangu na mimi ninaishi ndani yake. 57 Kama vile Baba wa uzima alivyonituma, na kama nipatavyo uzima kutoka kwake, kadhalika, ye yote anilaye ataishi kwa sababu yangu. 58 Huu ndio mkate uliotoka mbinguni, si kama ule mkate walio kula baba zenu hatimaye wakafa. Alaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sina gogi huko Kapernaumu.

Read full chapter