Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu

60 Wengi wa wanafunzi wake waliosikia maneno haya walisema, “Mafundisho haya ni magumu! Ni nani awezaye kukubaliana nayo?”

61 Yesu alitambua kwamba wafuasi wake walikuwa wakilalamika kuhusu mafundisho yake. Kwa hiyo akawauliza, “Mafundisho haya yanawaudhi? 62 Ingekuwaje basi, kama mngeniona mimi Mwana wa Adamu nikirudi mbinguni nilikotoka? 63 Roho wa Mungu ndiye anayetoa uzima, uwezo wa mwanadamu haufai kitu. Maneno haya ni Roho na ni uzima. 64 Lakini baadhi yenu hamuamini.” Kwa maana Yesu alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini na yule ambaye angemsaliti. 65 Akaendelea kusema, “Ndio sababu nili waambia kwamba hakuna awezaye kuja kwangu kama Baba hakumwe zesha.”

66 Tangu wakati huo wanafunzi wake wengi waliondoka wakaacha kumfuata.

Read full chapter

Wafuasi Wengi Wamwacha Yesu

60 Wafuasi wa Yesu waliposikia haya, wengi wao wakasema, “Fundisho hili ni gumu sana. Nani awezaye kulipokea?”

61 Yesu alikwishatambua kuwa wafuasi wake walikuwa wanalalamika juu ya hili. Hivyo akasema, “Je, fundisho hili ni tatizo kwenu? 62 Ikiwa ni hivyo mtafikiri nini mtakapomwona Mwana wa Adamu akipanda kurudi kule alikotoka? 63 Roho ndiye anayeleta uzima. Sio mwili. Lakini maneno niliyowaambia yanatoka kwa Roho, hivyo yanaleta uzima.” 64 Lakini baadhi yenu hamuamini. (Yesu aliwafahamu wale ambao hawakuamini. Alijua haya tangu mwanzo. Na alimjua yule ambaye angemsaliti kwa adui zake.) 65 Yesu akasema, “Ndiyo maana nilisema, ‘Hayupo hata mmoja ambaye anaweza kuja kwangu pasipo kusaidiwa na baba.’”

66 Baada ya Yesu kusema mambo hayo, wafuasi wake wengi wakamkimbia na wakaacha kumfuata.

Read full chapter