48 Mimi ni mkate wa uzima. 49 Baba zenu walikula mana jangwani, wakafa. 50 Lakini hapa kuna mkate utokao mbinguni ambao mtu ye yote akiula, hatakufa. 51 Mimi ni mkate wa uzima uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu ataishi milele. Na mkate wenyewe ni mwili wangu ambao nitautoa ili watu wote ulimwenguni wapate kuishi milele.”

52 Hapo Wayahudi wakaanza kubishana kwa hasira wakiulizana, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”

53 Kwa hiyo Yesu akasema, “Ninawaambieni hakika, msipoula mwili wangu mimi Mwana wa Adamu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. 54 Mtu ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. 55 Kwa maana mwili wangu ni chakula halisi na damu yangu ni kinywaji halisi. 56 Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu anaishi ndani yangu na mimi ninaishi ndani yake. 57 Kama vile Baba wa uzima alivyonituma, na kama nipatavyo uzima kutoka kwake, kadhalika, ye yote anilaye ataishi kwa sababu yangu. 58 Huu ndio mkate uliotoka mbinguni, si kama ule mkate walio kula baba zenu hatimaye wakafa. Alaye mkate huu ataishi milele.” 59 Yesu alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sina gogi huko Kapernaumu.

Read full chapter

48 Maana mimi ni mkate unaoleta uzima. 49 Baba zenu walikula mana waliyopewa na Mungu kule jangwani, lakini haikuwazuia kufa. 50 Hapa upo mkate unaotoka mbinguni. Yeyote anayekula mkate huu hatakufa kamwe. 51 Mimi ni mkate ulio hai ulioshuka kutoka mbinguni. Yeyote atakayeula mkate huu ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu. Nitautoa mwili wangu ili watu wa ulimwengu huu waweze kupata uzima.”

52 Kisha Wayahudi hawa wakaanza kubishana wao kwa wao. Wakasema, “Yawezekanaje mtu huyu akatupa mwili wake tuule?”

53 Yesu akasema, “Mniamini ninaposema kwamba mnapaswa kuula mwili wa Mwana wa Adamu, na mnapaswa kuinywa damu yake. Msipofanya hivyo, hamtakuwa na uzima wa kweli. 54 Wale wanaoula mwili wangu na kuinywa damu yangu wanao uzima wa milele. Nitawafufua siku ya mwisho. 55 Mwili wangu ni chakula halisi, na damu yangu ni kinywaji halisi. 56 Wale waulao[a] mwili wangu na kuinywa damu yangu wanaishi ndani yangu, nami naishi ndani yao.

57 Baba alinituma. Yeye anaishi, nami naishi kwa sababu yake. Hivyo kila anayenila mimi ataishi kwa sababu yangu. 58 Mimi siyo kama ule mkate walioula baba zenu. Wao waliula mkate huo, lakini bado walikufa baadaye. Mimi ni mkate uliotoka mbinguni. Yeyote atakayeula mkate huu ataishi milele.”

59 Yesu aliyasema haya yote alipokuwa akifundisha kwenye Sinagogi katika mji wa Kapernaumu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 6:56 waulao Kukaa kula Maana yake, “kutafuna kwa kelele” au “kutafuna kwa nguvu”. Ni neno la kufurahia kula, kunywa na ushirika baada ya mlo mkuu. Sehemu hii ya mlo pia ilijulikana kama “meza ya pili”.