Yesu Amponya Mtu Penye Bwawa La Bethzatha

Baada ya haya, Yesu alikwenda tena Yerusalemu kuhudhuria sikukuu mojawapo ya Wayahudi. Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, pana bwawa moja ambalo kwa Kiebrania linaitwa Bethzatha ambalo lina baraza tano zenye safu za matao. Wagonjwa wengi sana, vipofu, viwete, na waliopooza walingojea kwenye baraza hizo. Walikuwa wakisubiri maji yatibuliwe, [ kwa maana malaika wa Bwana alikuja mara kwa mara akayatibua maji na yule aliyekuwa wa kwanza kuingia bwawani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wo wote aliokuwa nao.]

Mmoja wa wagonjwa waliokuwepo alikuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alipomwona amelala hapo, na akijua kwamba amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, alimwul iza, “Unataka kupona?” Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Ninapoanza kwenda bwawani, mgonjwa mwingine huniwahi akaingia kabla yangu.” Yesu akamwambia, “Simama, chukua mkeka wako, utembee!” Mara moja yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea! Jambo hili lilitokea siku ya sabato. 10 Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni sabato. Huruhusiwi kubeba mkeka wako.”

11 Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chu kua mkeka wako utembee.”’

12 Wakamwuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako utembee?”

13 Yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya kwa sababu palikuwa na umati mkubwa wa watu na Yesu alikuwa amepe nyezea humo akaondoka.

14 Baadaye Yesu alimkuta yule aliyemponya Hekaluni akamwam bia, “Sasa umepona. Angalia usitende dhambi tena usijepatwa na jambo baya zaidi.”

15 Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.

16 Kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya sabato, wal ianza kumsumbua. 17 Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya mema siku zote. Mimi pia sina budi kufanya mema.” 18 Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate kumwua, kwa sababu, zaidi ya kuvunja sheria za sabato, alikuwa akijifanya sawa na Mungu kwa kujiita Mwana wa Mungu.

Read full chapter

Yesu Amponya Mtu Bwawani

Baadaye, Yesu akaenda Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu maalumu ya Wayahudi. Huko Yerusalemu kulikuwa na bwawa lenye mabaraza matano. Kwa Kiaramu liliitwa Bethzatha.[a] Bwawa hili lilikuwa karibu na Lango la Kondoo. Wagonjwa wengi walikuwa wamelala katika mabaraza pembeni mwa bwawa. Baadhi yao walikuwa wasiyeona, wengine walemavu wa viungo, na wengine waliopooza mwili.[b] Nyakati zingine malaika wa Bwana alishuka bwawani na kuyatibua maji. Baada ya hapo, mtu wa kwanza aliyeingia bwawani aliponywa ugonjwa aliokuwa nao.[c] Mmoja wa watu waliolala hapo alikuwa mgonjwa kwa muda wa miaka thelathini na minane. Yesu alimwona akiwa amelala hapo na kutambua kuwa amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sana. Hivyo akamwuliza, “Je, unataka kuwa mzima?”

Yule mgonjwa akajibu, “Bwana, hakuna mtu wa kunisaidia kuingia kwenye bwawa mara maji yanapotibuliwa. Najitahidi kuwa wa kwanza kuingia majini. Lakini ninapojaribu, mtu mwingine huniwahi na kuingia majini kabla yangu.”

Kisha Yesu akasema, “Simama juu! Beba kirago chako na utembee.” Mara hiyo, mtu huyo akapona. Akabeba kirago chake na kuanza kutembea.

Siku yalipotokea haya yote ilikuwa ni Siku ya Sabato.[d] 10 Hivyo baadhi ya Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato. Kulingana na sheria yetu wewe hauruhusiwi kubeba mkeka katika siku ya Sabato!”

11 Lakini yeye akajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Beba mkeka wako uende.’”

12 Wakamwuliza, “Ni nani aliyekuambia kubeba mkeka wako na kutembea?”

13 Lakini yule mtu aliyeponywa hakuwa amemfahamu ni nani. Walikuwepo watu wengi hapo, na Yesu alikwisha kuondoka.

14 Baadaye, Yesu akamwona huyo mtu Hekaluni na akamwambia, “Tazama, umepona sasa. Kwa hivyo uache kutenda dhambi tena, la sivyo jambo baya zaidi laweza kukupata.” 15 Kisha huyo mtu akaondoka na kurudi kwa wale Wayahudi waliomuuliza. Naye aliwaeleza kuwa Yesu ndiye aliyemponya.

16 Yesu alikuwa anayafanya yote haya katika siku ya Sabato. Hivyo Wayahudi hao wakaanza kumsumbua asiendelee. 17 Lakini yeye akawaambia, “Baba yangu hajawahi kuacha kufanya kazi, hivyo nami pia nafanya kazi.” 18 Hili likawafanya waongeze juhudi ya kumwua. Wakasema, “Mwanzoni mtu huyu alikuwa anavunja sheria kuhusu siku ya Sabato. Kisha akasema kwamba Mungu ni Baba yake! Yeye anajifanya kuwa yuko sawa na Mungu.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:2 Bethzatha Pia huitwa Bethsaida au Bethesda. Ama bwawa la maji lililoko kaskazini mwa Hekalu kule.
  2. 5:3 Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza, “na husubiri maji yatibuliwe”.
  3. 5:4 Nakala zingine za baadaye ziliongeza mstari wa 4, hivyo kutenganisha mstari wa 4 na wa 5: “Nyakati zingine malaika wa Bwana alishuka bwawani na kuyatibua maji. Baada ya hapo, mtu wa kwanza aliyeingia bwawani aliponywa ugonjwa aliokuwa nao.”
  4. 5:9 Siku ya Sabato Ilikuwa siku maalumu kwa Waisraeli na Wayahudi. Kwa amri ya Mungu siku hiyo ilitengwa kama siku ya mapumziko na ya kumheshimu Mungu.