Basi ilikuwapo hapo mitungi sita ya kuwekea maji ya kunawa, kufuatana na desturi ya Wayahudi ya kutawadha. Kila mtungi ungeweza kujazwa kwa madebe sita au saba ya maji. Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu. Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai. Hakujua divai hiyo imetoka wapi ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana harusi kando 10 akamwambia, “Watu wote huwapa wageni divai nzuri kwanza kisha wakianza kutosheka huwaletea divai hafifu.

Read full chapter

Mahali hapo ilikuwepo mitungi mikubwa sita iliyotengenezwa kwa mawe iliyotumiwa na Wayahudi katika desturi yao maalumu ya kunawa.[a] Kila mtungi mmoja ulikuwa na ujazo wa lita 80 au 120.[b]

Yesu akawaambia wale wahudumu, “Ijazeni maji hiyo mitungi.” Nao wakaijaza maji mpaka juu.

Kisha akawaambia, “Sasa choteni hayo maji kiasi na mumpelekee mkuu wa sherehe.” Nao wakafanya kama walivyoambiwa. Mkuu wa sherehe akayaonja yale maji, ambayo tayari yamegeuka na kuwa divai. Naye hakujua wapi ilikotoka hiyo divai, bali wahudumu walioleta yale maji wao walijua. Akamwita bwana arusi 10 na kumwambia, “Watu wanapoandaa huleta kwanza divai iliyo bora zaidi. Baadaye, wageni wanapokuwa wametosheka, huleta divai iliyo na ubora pungufu. Lakini wewe umeandaa divai bora zaidi hadi sasa.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 2:6 desturi yao maalumu ya kunawa Wayahudi walikuwa na sheria za kidini za kunawa maji kwa namna maalumu kabla ya kula, kabla ya kufanya ibada katika Hekalu, na pia nyakati zingine maalumu.
  2. 2:6 lita 80 au 120 Kwa maana ya kawaida, “metretas 2 au 3”.