29 Hapo palikuwa na bakuli lililojaa siki. Kwa hiyo wakachukua sponji iliyolowanishwa kwenye hiyo siki wakaichomeka kwenye ufito wa hisopo wakampandishia mdomoni. 30 Baada ya kuipokea hiyo siki, Yesu akasema, “Imekwisha.” Akainamisha kichwa, akakata roho.

Read full chapter

29 Palikuwapo na bakuli lililojaa siki[a] mahali pale, wale askari wakachovya sponji ndani yake. Wakaiweka ile sponji kwenye tawi la mwanzi na kuliinua hadi kinywani kwa Yesu. 30 Alipoionja ile siki, akasema, “Imekwisha.” Baada ya hapo akainamisha kichwa chake na kufa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 19:29 siki Divai chungu; yaani, siki ya mvinyo (au divai chungu) uliochanganywa na maji. Hiki kilikuwa kinywaji rahisi na kilichojulikana sana wakati wa Yesu.