Kisha akamimina maji katika chombo akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa ile taulo aliyojifunga kiu noni. Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, wewe unaniosha miguu?” Yesu akamjibu, “Hivi sasa huelewi ninalofa nya lakini baadaye utaelewa.” Petro akamjibu, “La, hutaosha miguu yangu kamwe!” Yesu akamwambia, “Kama sitaosha miguu yako, huwezi kuwa mfuasi wangu.” Ndipo Petro akasema, “Kama ni hivyo Bwana, nioshe miguu yangu pamoja na mikono yangu na kichwa changu pia!” 10 Yesu akamwambia, “Mtu aliyekwishaoga ni safi mwili mzima naye hahitaji tena kunawa ila kuosha miguu tu. Ninyi nyote ni safi, isipokuwa mmoja.” 11 Yesu alifahamu ni nani angemsaliti, ndio sababu akasema, “Ninyi nyote ni safi, isipo kuwa mmoja.”

12 Alipomaliza kuwaosha miguu alivaa tena vazi lake, akarudi alipokuwa amekaa, ndipo akawaambia, “Je, mnaelewa maana ya jambo nililowafanyia? 13 Ninyi mnaniita mimi, Mwalimu na Bwana, na hii ni sawa, kwani ni kweli. 14 Kwa hiyo ikiwa mimi niliye Bwana wenu na Mwalimu wenu nimewaosha miguu, ninyi pia hamna budi kuoshana miguu.

Read full chapter