alitoka mezani akaweka vazi lake kando, akajifunga taulo kiunoni. Kisha akamimina maji katika chombo akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuikausha kwa ile taulo aliyojifunga kiu noni. Alipomfikia Simoni Petro, Petro akamwambia, “Bwana, wewe unaniosha miguu?” Yesu akamjibu, “Hivi sasa huelewi ninalofa nya lakini baadaye utaelewa.” Petro akamjibu, “La, hutaosha miguu yangu kamwe!” Yesu akamwambia, “Kama sitaosha miguu yako, huwezi kuwa mfuasi wangu.” Ndipo Petro akasema, “Kama ni hivyo Bwana, nioshe miguu yangu pamoja na mikono yangu na kichwa changu pia!” 10 Yesu akamwambia, “Mtu aliyekwishaoga ni safi mwili mzima naye hahitaji tena kunawa ila kuosha miguu tu. Ninyi nyote ni safi, isipokuwa mmoja.” 11 Yesu alifahamu ni nani angemsaliti, ndio sababu akasema, “Ninyi nyote ni safi, isipo kuwa mmoja.”

Read full chapter

Kwa hiyo walipokuwa wakila,[a] Yesu alisimama na kulivua vazi lake. Akachukua taulo na kuifunga kiunoni mwake. Kisha akamimina maji katika bakuli na kuanza kuwaosha miguu[b] wafuasi wake. Kisha akaifuta miguu yao kwa taulo aliolifunga kiunoni mwake.

Akamfikia Simoni Petro, naye Simoni Petro akamwambia, “Bwana, huwezi kuiosha miguu yangu.”

Yesu akamjibu, “Huyaelewi ninayofanya hivi sasa. Lakini utayaelewa baadaye.”

Petro akasema, “Hapana! Huwezi kamwe kuniosha miguu yangu kamwe.”

Yesu akamjibu, “Kama sitakuosha miguu yako, basi hutakuwa miongoni mwa watu wangu.”

Simoni Petro akasema, “Bwana, utakapomaliza miguu, unioshe mikono na kichwa pia!”

10 Yesu akamwambia, “Baada ya mtu kuoga, mwili wake wote huwa safi. Anahitaji tu kunawa miguu. Nanyi mko safi, lakini sio nyote.” 11 Yesu alimjua yule atakayemsaliti mbele ya adui zake. Ndiyo maana alisema, “Sio wote mlio safi.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 13:4 wakila Wafuasi walikuwa kwenye makochi, wakiwa wameegemea kushoto kwao, na wakitumia mikono ya kulia kufikia vyombo vilivyokuwa mezani, vilivyowekwa mbele ya makochi. Yesu akamimina maji kwenye “jagi” (Wayunani huelezea kuwa hiki kilikuwa chombo kilichotumika maalumu kwa kusudi hilo) na kisha akaenda akimpitia mmoja mmoja nyuma ya kochi, ambako miguu ya wafuasi ilikuwa imenyooshwa.
  2. 13:5 kuwaosha miguu Utaratibu wa kijamii wa karne ya kwanza, kwa sababu watu walivaa viatu vya wazi katika barabara za vumbi jingi. Ulikuwa ni wajibu wa unyenyekevu, kawaida uliofanywa na mtumishi. Pia katika mstari wa 6-14.