Mariamu Ampaka Yesu Mafuta

12 Siku sita kabla ya sikukuu ya Pasaka, Yesu alikwenda mpaka Bethania ambako Lazaro aliyemfufua alikuwa anaishi. Wakamwan dalia karamu; na Martha akawahudumia. Lazaro alikuwa miongoni mwa wageni waliokaa mezani pamoja na Yesu. Kisha Mariamu akachukua chupa yenye manukato ya thamani kubwa akayamimina miguuni mwa Yesu na kuipangusa kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu ya manukato. Ndipo Yuda Iskariote, mmoja wa wanafunzi, ambaye baadaye alimsaliti Yesu, akasema, “Kwa nini manukato haya hay akuuzwa zikapatikana fedha nyingi wapewe maskini?” Yuda alisema hivi si kwa kuwa aliwajali sana maskini bali kwa kuwa alikuwa mwizi. Kama mtunza fedha, alikuwa mara kwa mara anaiba kutoka katika fedha alizokabidhiwa. Yesu akajibu, “Msimsumbue! Mwacheni ayaweke manukato hayo kwa ajili ya siku ya kifo changu. Maskini wapo pamoja nanyi siku zote ila hamtakuwa nami siku zote. ”

Read full chapter