Add parallel Print Page Options

36 Hivyo wekeni matumaini yenu katika nuru wakati bado mkiwa nayo. Jinsi hiyo mtakuwa watoto wa nuru.” Yesu alipomaliza kusema mambo hayo, aliondoka na kwenda mahali ambapo watu wasingeweza kumwona.

Baadhi ya Wayahudi Wakataa Kumwamini Yesu

37 Watu wakaona ishara[a] hizi zote alizozifanya Yesu, lakini bado hawakumwamini. 38 Haya yalikuwa hivyo ili kuthibitisha yale aliyoyasema nabii Isaya kuwa:

“Bwana, ni nani aliyeamini yale tuliyowaambia?
    Ni nani aliyeziona nguvu za Bwana?”(A)

39 Hii ndiyo sababu watu hawakuweza kuamini. Kwani Isaya alisema pia,

40 “Mungu aliwafanya baadhi ya watu wasione.
    Aliufunga ufahamu wao.
Alifanya hivi ili wasiweze kuona kwa macho yao
    na kuelewa kwa ufahamu wao.
Alifanya hivyo ili wasiweze kugeuka
    na kuponywa.”(B)

41 Isaya alisema hivi kwa sababu aliuona ukuu wa Mungu[b] ndani ya Yesu. Naye alizungumza habari zake Yesu.

42 Lakini watu wengi wakamwamini Yesu. Hata wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi wakamwamini, lakini walikuwa na hofu juu ya Mafarisayo, hivyo hawakusema kwa uwazi kwamba wameamini. Hao walikuwa na hofu kwamba wangeamriwa watoke na kukaa nje ya sinagogi. 43 Wao walipenda kusifiwa na watu zaidi kuliko kupata sifa zinazotoka kwa Mungu.

Read full chapter

Footnotes

  1. 12:37 ishara Ni tendo la kushangaza linalodhihirisha nguvu za Mungu.
  2. 12:41 Mungu Kihalisia, “utukufu”, ni neno linaloonyesha sifa maalumu za Mungu. Tazama Utukufu katika Orodha ya Maneno.