11 Mimi ni Mchungaji Mwema. Mchungaji Mwema hutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtu wa kuajiriwa anapoona mbwa mwitu akija, hukimbia na kuwaacha kondoo hatarini kwa kuwa kondoo si wake, naye si mchungaji wao; na hivyo mbwa mwitu huwar ukia kondoo na kuwatawanya. 13 Yeye hukimbia kwa sababu ameaji riwa tu na hawajali kondoo.

14 Mimi ni Mchungaji Mwema: ninawafahamu kondoo wangu nao wananifahamu, 15 kama vile Baba yangu anavyonifahamu na mimi ninamfahamu. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. 16 Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili; nao pia itanibidi niwalete, nao wataisikia sauti yangu. Hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja. 17 Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena. 18 Hakuna mtu atakayeondoa uhai wangu, bali ninautoa mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu na pia ninao uwezo wa kuuchukua tena. Hii ni amri niliyopo kea kutoka kwa Baba yangu.”

Read full chapter