Kama kweli mnatimiza ile sheria ya kifalme iliyomo katika Maandiko, “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe,” mnafanya vema. Lakini kama mnafanya ubaguzi, mna tenda dhambi na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji. 10 Kwa maana mtu ye yote anayetimiza sheria yote isipokuwa akashindwa kutimiza sehemu moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote. 11 Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini” ndiye huyo huyo aliyesema, “Usiue.” Kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria yote.

12 Kwa hiyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria iletayo uhuru. 13 Maana hukumu haina huruma kwa mtu asi yekuwa na huruma. Lakini huruma huishinda hukumu.

Read full chapter