Yesu alipokuwa akiishi duniani, alitoa dua na maombi kwa kilio kikuu na machozi kwa Mungu ambaye angeweza kumwokoa na kumtoa katika kifo, naye Mungu alimsikia kwa sababu alikuwa mnyenyekevu na mtiifu. Ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, aliji funza utii kutokana na mateso aliyopata; na baada ya kufanywa mkamilifu, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii,

Read full chapter

Yesu alipoishi duniani alimwomba Mungu, akiusihi msaada kutoka kwa yule anayeweza kumwokoa kutoka mauti. Alimwomba Mungu kwa sauti kuu na kwa machozi. Na Mungu alizisikia sala zake kwa sababu ya heshima yake kuu kwa Mungu. Yesu alikuwa mwana wa Mungu, lakini aliteseka, na kwa njia ya mateso yake alijifunza kutii chochote alichosema Mungu. Hili lilimfanya yeye awe kuhani mkuu mkamilifu, anayetoa njia kwa ajili ya kila mmoja anayemtii ili kuokolewa milele.

Read full chapter