Kuhani Mkuu Yesu Kristo

14 Hivyo basi, kwa kuwa tunaye kuhani mkuu aliyepitia mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, tushikilie kwa uthabiti imani yetu tunayoikiri. 15 Kwa maana huyu kuhani wetu mkuu si kuhani ambaye hawezi kutuhurumia katika udhaifu wetu, bali ni kuhani ambaye kwa kila hali amejaribiwa kama sisi, lakini pasipo kutenda dhambi.

Read full chapter