Hatari Ya Kukufuru

26 Kama tukiendelea kutenda dhambi makusudi baada ya kupokea na kufahamu ile kweli, hakuna tena dhabihu iliyobaki inayoweza kutolewa kwa ajili ya dhambi. 27 Kinachobakia ni kungojea kwa hofu hukumu ya Mungu na moto mkali utakaowaangamiza maadui zake. 28 Mtu aliyevunja sheria ya Mose aliuawa pasipo huruma kwa usha hidi wa watu wawili au watatu. 29 Je, mnadhani ni adhabu kali kiasi gani zaidi anastahili kupewa mtu ambaye anamdharau na kum kataa Mwana wa Mungu, na ambaye anaona kuwa damu ya agano iliyom takasa si kitu, na ambaye amemtukana Roho wa neema?

Read full chapter