23 Kabla imani haijakuwepo tulikuwa tumefungwa chini ya sheria, mpaka imani ifunuliwe. 24 Kwa hiyo, sheria ilikuwa kama kiongozi wa kutufikisha kwa Kristo, ili tuhesabiwe haki kwa imani. 25 Lakini sasa kwa kuwa imani imekuja hatusimamiwi tena na sheria.

Read full chapter

23 Kabla ya aliye mwaminifu kuja, sheria ilituweka sisi kama wafungwa. Hatukuwa huru hadi imani hii inayokuja[a] ilipofunuliwa kwetu. 24 Nina maana kuwa sheria ilikuwa ni mlezi aliyetusimamia[b] tu hadi Kristo alipokuja. Baada ya kuja kwake, tungefanyika kuwa wenye haki mbele za Mungu kwa njia ya imani. 25 Sasa kwa sababu imani hii imekuja, hatuhitaji tena kusimamiwa na kulelewa na sheria.

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:23 imani hii inayokuja Au “imani ya Yesu”.
  2. 3:24 mlezi aliyetusimamia Ina maana kama ile ya mlezi wa watoto yaani yaya; Kwa Kiyunani namaanisha mtu, kwa kawaida aliyekuwa mtumwa, aliyemsindikiza mvulana mdogo kwenda shule toka nyumbani na kuhakikisha ya kwamba mvulana yule anaenenda vizuri na hapati matatizo.