Nilikwenda kwa sababu nilikuwa nimefunuliwa na Mungu, kwamba nikawaeleze kwa faragha wale waliokuwa viongozi, Injili ninayohubiri kwa watu wa mataifa mengine. Nilifanya hivyo ili kazi yangu niliyokwisha fanya na hii ninayofanya sasa isije ikawa bure. Hata hivyo Tito ambaye alikuwa ni Mgiriki, hakulazimika kutahiriwa. Lakini walikuwepo ndugu wengine wa uongo ambao walikuja kwa siri kupeleleza uhuru tulio nao katika Kristo Yesu, ili waturudishe kwenye utumwa wa sheria. Sisi hatukukubaliana nao hata kidogo ili ukweli wa Injili uendelee kutunzwa kwa ajili yenu.

Read full chapter