Kuokoka Kwa Sauli

Wakati huu wote Sauli alikuwa bado anaendelea na vitisho vyake vya kuwaangamiza kabisa wanafunzi wa Bwana. Akaenda kwa Kuhani Mkuu, akamwomba ampe barua ya kumtambulisha kwa masina gogi ya huko Dameski, ili akiwapata wafuasi wa ile ‘Njia Basi katika safari yake, alipokuwa akikaribia Dameski, ghafla nuru kutoka mbinguni iliangaza kumzunguka! Akaanguka chini! Na aka sikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona unanitesa?” Sauli akajibu, “Ni nani wewe, Bwana?” Ile sauti ikasema, “Mimi ni Yesu ambaye unamtesa. Lakini sasa inuka uingie mjini nawe utaambiwa la kufanya.” Wale waliokuwa wakisafiri na Sauli wakasimama kwa mshangao, wala hawakuweza kusema neno kwa sababu walisikia sauti lakini hawakumwona aliyekuwa akizungumza. Sauli akainuka na alipojaribu kufungua macho, hakuweza kuona kitu. Basi wakamshika mkono wakamwongoza mpaka Dameski. Na kwa muda wa siku tatu akawa haoni kabisa, na hakula kitu wala kunywa cho chote.

10 Huko Dameski alikuwepo mfuasi mmoja jina lake Anania. Bwana akamwita Anania katika ndoto, “Anania! ” Akaitika, “Nipo hapa Bwana.” 11 Bwana akamwambia, “Amka uende barabara iitwayo Nyofu ukaulizie katika nyumba ya Yuda kuhusu mtu aitwaye Sauli wa Tarso. Yeye hivi sasa anaomba, na katika maono anamwona mtu 12 aitwaye Anania akija na kuweka mikono juu yake ili aweze kuona tena.” 13 Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi mambo ya kutisha ambayo mtu huyu anawatendea wataka tifu wako huko Yerusalemu. 14 Naye amekuja hapa Dameski akiwa na kibali kutoka kwa Kuhani Mkuu awakamate wote wanaotaja jina lako.” 15 Lakini Bwana akamwambia Anania, “Nenda, kwa maana nimemchagua awe mtumishi wangu wa kulitangaza jina langu kwa mataifa na wafalme na kwa wana wa Israeli; 16 nami nitamwonyesha atakavyoteseka sana kwa ajili ya jina langu .” 17 Anania akaenda, akaingia mle nyumbani. Akaweka mikono yake juu ya Sauli akasema, “Ndugu yangu Sauli, Bwana Yesu aliyekutokea njiani ame nituma kwako ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.” 18 Mara vitu kama magamba vikaanguka kutoka machoni mwa Sauli, akapata kuona tena. Akasimama, akabatizwa. 19 Kisha akala chak ula, akapata nguvu tena. Alikaa siku kadhaa pamoja na wanafunzi huko Dameski na

Read full chapter