Filipo Ambatiza Afisa Wa Ethiopia

26 Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Nenda upande wa kusini kwenye ile barabara itokayo Yerusalemu kuelekea Gaza.” Hii ilikuwa barabara iendayo jangwani. 27 Filipo akaondoka akaenda. Wakati huo Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa waziri wa fedha wa Kandake, Malkia wa Ethiopia, alikuwa anarudi nyumbani baada ya kumwabudu Mungu huko Yerusalemu. 28 Alikuwa amekaa kwenye gari la kuvutwa na farasi akielekea makwao, akisoma kitabu cha nabii Isaya. 29 Roho wa Mungu akamwambia Filipo, “Nenda kasimame karibu na lile gari.” 30 Kwa hiyo Filipo aka harakisha kulikaribia, na alipofika karibu akamsikia yule afisa akisoma katika kitabu cha nabii Isaya, akamwuliza, “Je, unaelewa unachosoma?” 31 Yule afisa akamjibu, “Nitaelewaje mtu asipo nielekeza? Akamkaribisha Filipo katika gari, akaketi pamoja naye. 32 Maneno aliyokuwa akisoma ni haya, ‘Alipelekwa kama kon doo anayetolewa kuchinjwa na kama mwana-kondoo anavyotulia anapo katwa manyoya, naye hakusema neno lo lote. 33 Aliaibishwa, aka nyimwa haki yake. Ni nani awezaye kuelezea juu ya kizazi chake? Kwa maana uhai wake umeondolewa duniani.’ 34 Yule towashi akam wuliza Filipo, “Tafadhali niambie, Isaya alikuwa akisema haya juu yake mwenyewe au juu ya mtu mwingine?” 35 Ndipo Filipo akaanza kusema naye, akitumia Maandiko haya akamweleza Habari Njema za Yesu. 36 Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, na yule towashi akamwambia Filipo, “ Tazama, hapa kuna maji! Kuna kitu gani cha kunizuia mimi nisiba tizwe? [ 37 Filipo akamwambia, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”] 38 Akaamuru gari lisimamishwe. Wakateremka, yule towashi na Filipo, wakaenda pale kwenye maji. Filipo akamba tiza. 39 Walipotoka katika yale maji, Roho wa Bwana akamchukua Filipo na yule towashi hakumwona tena. Kwa hiyo akaendelea na safari yake akiwa amejawa na furaha. 40 Filipo akajikuta yuko Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipo fika Kaisaria.

Read full chapter