Stefano Auawa Kwa Kupigwa Mawe

54 Basi wale viongozi waliposikia maneno haya walijawa na hasira, wakasaga meno yao kwa ghadhabu. 55 Lakini Stefano akiwa amejawa na Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, akamwona Yesu amesimama upande wa kulia wa Mungu.” 56 Akasema, “Tazameni! Naona mbingu zimefunguka na Mwana wa Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

Adamu amesimama upande wa kulia wa Mungu.”

57 Wao wakapiga makelele, wakaziba masikio yao wasimsikie, wakamrukia kwa pamoja. 58 Wakamtupa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Na mashahidi walioteuliwa walimwachia kijana mmoja aitwae Sauli mavazi yao. 59 Walipokuwa wakimpiga mawe, Stefano aliomba, Bwana Yesu, pokea roho yangu!” 60 Akapiga magoti akalia kwa sauti kubwa akasema, “Bwana usiwahesabie dhambi hii.” Baada ya kusema haya, akafa.

Na Sauli aliunga mkono kuuawa kwa Stefano Tangu siku hiyo waamini katika kanisa la Yerusalemu walianza kuteswa sana. Waamini wote isipokuwa mitume wakatawanyika, wakakimbilia katika majimbo ya Yudea na Samaria. Watu waliomcha Mungu walimzika Stefano na kumwombolezea sana. Lakini Sauli alitaka kulianga miza kanisa kabisa. Akawa akienda kila nyumba akawaburura waamini, wanaume kwa wanawake, akawatia jela.

Injili Yahubiriwa Samaria

Wale waamini waliotawanyika walihubiri neno la Mungu kila mahali walipokuwa. Filipo naye alikwenda katika mji mmoja wa Samaria akahubiri habari za Kristo. Watu wengi walipomsikiliza Filipo na kuona ishara za ajabu alizofanya, walizingatia kwa makini ujumbe wake. Pepo wachafu walikuwa wakiwatoka watu wengi, huku wakipiga makelele; na wengi waliopooza na viwete, waliponywa. Pakawa na furaha kuu katika mji huo.