23 Musa alipokuwa na umri wa miaka arobaini akawa na hamu ya kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. 24 Alipoona mmoja wao akionewa na Mmisri, akamwua yule Mmisri kulipiza kisasi. 25 Alidhani kuwa ndugu zake wangeelewa kwamba Mungu ali kuwa akiwaokoa kwa msaada wake, lakini wao hawakuelewa. 26 Kwa hiyo siku ya pili alipoona Waisraeli wanagombana alijaribu kuwa patanisha, akawaambia, ‘Jamani, ninyi ni ndugu. Mbona mnaoneana wenyewe kwa wenyewe?’ 27 Lakini yule aliyekuwa akimwonea mwen zake akamsukumia Musa kando, akamwuliza, ‘Ni nani aliyekuweka uwe mtawala na mwamuzi kati yetu? 28 Je, unataka kuniua kama ulivy omwua yule Mmisri jana?’ 29 Musa aliposikia maneno haya alikim bia akatoka Misri akaenda kuishi kama mkimbizi sehemu za Midiani. Huko akawa baba wa watoto wawili wa kiume. 30 “Baada ya miaka arobaini, malaika wa Mungu akamtokea jangwani karibu na Mlima Sinai katika kichaka kilichokuwa kina waka moto.

Read full chapter