Stefano Akamatwa

Na Stefano akiwa amejawa na neema na nguvu za Mungu alifa nya maajabu makubwa na ishara kati ya watu.

Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa la ‘Watu Huru,’ na wengine kutoka masinagogi ya Kirene na Aleksandria, pamoja na baadhi kutoka Kilikia na Asia, wakajaribu kubishana na Stefano. 10 Lakini hawakuweza kushindana naye kwa sababu ya hekima yake na Roho aliyemwezesha kusema.

11 Ndipo wakawashawishi watu fulani ambao walisema, “Tulim sikia akisema maneno ya kufuru juu ya Musa na Mungu.”

Stefano Afikishwa Mbele Ya Baraza

12 Wakawachochea watu, wazee na waandishi wa sheria nao wakamkamata Stefano wakamfikisha mbele ya baraza. 13 Wakaweka mashahidi wa uongo ambao walisema, “Mtu huyu siku zote anasema maneno ya kashfa juu ya Hekalu hili takatifu na juu ya sheria za Musa. 14 Kwa maana tumemsikia akisema kwamba eti huyu Yesu wa Nazareti ataharibu hili Hekalu takatifu na atabadilisha mila zote tulizopewa na Musa.”

Read full chapter