Ushirika Wa Waamini

42 Waamini hawa walitumia muda wao wakifundishwa na mitume, wakiishi pamoja katika ushirika, wakila pamoja na kusali. 43 Watu wote wakajawa na hofu kwa maana miujiza mingi na maajabu yalifanywa na mitume.

44 Waamini wote waliishi pamoja na kushirikiana kila kitu walichokuwa nacho kwa pamoja. 45 Waliuza mali zao na vitu waliv yokuwa navyo wakagawiana fedha walizopata, kila mtu akapata kadiri ya mahitaji yake. 46 Siku zote waliendelea kuabudu katika Hekalu na kushiriki chakula cha Bwana nyumbani mwao na kula pamoja kwa furaha na shukrani, 47 huku wakimsifu Mungu na kupendwa na watu wote. Na kila siku Bwana alikuwa akiongeza katika kundi lao watu aliokuwa akiwaokoa.

Read full chapter