31 Walipokuwa wakitaka kum wua, habari zikamfikia Jemadari wa jeshi la askari wa Kirumi kwamba Yerusalemu yote ilikuwa katika hali ya machafuko. 32 Na mara yule jemadari akachukua maofisa wengine wa jeshi pamoja na maaskari wakakimbilia kwenye ile ghasia. Watu walipomwona jema dari na askari wakija, waliacha kumpiga Paulo. 33 Kisha yule jemadari akamkamata Paulo akaamuru afungwe kwa minyororo miwili. Akauliza yeye ni nani na alikuwa amefanya nini. 34 Baadhi ya watu wakapiga kelele wakieleza jambo moja na wengine wakieleza jingine. Yule jemadari alipoona kuwa hawezi kupata ukweli kamili kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo apelekwe katika ngome ya jeshi. 35 Basi walipofika penye ngazi, ilibidi askari wambebe Paulo juu juu kwa sababu ya fujo za ule umati wa watu 36 ambao walikuwa wakiwafuata wakipiga kelele, “Mwueni!”

Paulo Anajitetea

37 Walipokuwa wanakaribia kuingia katika ngome ya jeshi, Paulo alimwuliza yule jemadari, “Je, naweza kusema jambo moja?” Yule jemadari akajibu, “Kumbe unajua Kigiriki? 38 Wewe si yule Mmisri ambaye siku za karibuni alianzisha uasi akaongoza majam bazi elfu nne wenye silaha jangwani?” 39 Paulo akajibu, “Mimi ni Myahudi, mzaliwa wa Tarso, jimbo la Kilikia na raia wa mji wenye sifa. Tafadhali niruhusu nizungumze na hawa watu.” 40 Yule jemadari alipomruhusu azungumze, Paulo akasimama penye ngazi akawapungia watu mkono ili wanyamaze. Watu walipokuwa kimya kabisa, Paulo akazungumza nao kwa lugha ya Kiebrania, akasema;

Ushuhuda Wa Paulo Kwa Wayahudi Wa Yerusalemu

22 “Ndugu zangu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu.” Waliposikia akisema kwa lugha ya Kiebrania, wakatulia zaidi, naye akasema, “Mimi ni Myahudi, niliyezaliwa Tarso huko Kili kia, lakini nimekulia hapa Yerusalemu, nikiwa mwanafunzi wa Gamalieli. Nilielimishwa kwa kufuata utaratibu maalumu wa sheria za baba zetu, nikiwa na ari ya kumheshimu Mungu kama ninyi mlivyo siku hii ya leo. Niliwatesa wafuasi wa ‘Njia’ mpaka wakafa. Niliwakamata, waume kwa wake, nikawafunga na kuwaweka gerezani. Kuhani mkuu na baraza zima la wazee ni mashahidi wangu kuhusu jambo hili. Wao ndio walionipa barua za kupeleka kwa ndugu zao huko Dameski. Kwa hiyo nilikwenda kuwakamata wafuasi wa ‘Njia’ niwalete Yerusalemu kama wafungwa ili waadhibiwe. Nilipokuwa nimekaribia kufika Dameski, mnamo muda wa kama saa sita mchana, kulitokea mwanga mkali kutoka mbinguni ukaangaza pande zote kuni zunguka. Nikaanguka chini, nikasikia sauti ikiniambia, ‘Sauli! Sauli! Mbona unanitesa?’ Nikajibu, ‘Wewe ni nani Bwana?’ Naye akajibu, ‘Mimi ni Yesu wa Nazareti unayemtesa.’

“Wale watu niliokuwa nikisafiri nao waliona ule mwanga, lakini hawakuelewa ile sauti ya yule aliyekuwa akisema nami. 10 Nikauliza, ‘Nifanye nini Bwana?’ Naye Bwana akaniambia, ‘Inuka uingie Dameski na huko utaambiwa mambo yote uliyopangiwa kufanya.’ 11 Nilikuwa sioni kwa sababu ya ule mwanga mkali kwa hiyo wenzangu wakanishika mkono wakaniongoza na hivyo tukafika Dameski. 12 “Mtu mmoja aitwaye Anania, mtu wa dini, aliyeshika sana sheria zetu, na ambaye aliheshimiwa sana na Wayahudi wote wa Dameski, 13 alinijia akasimama karibu yangu akasema, ‘Ndugu Sauli, pokea tena uwezo wa kuona!’ Na wakati ule ule nikaweza kuona tena, nikamwona Anania. 14 Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe ufahamu mapenzi yake, umwone yeye Mwenye Haki na usikie akisema nawe kwa sauti yake mwenyewe. 15 Kwa kuwa utakuwa shahidi wake kwa watu wote uwaambie yote uliyoyaona na kuyasikia. 16 Sasa basi, mbona unakawia? Simama ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako kwa kuliitia jina lake.” ’

Wito Wa Paulo Kuwahubiri Mataifa

17 “Niliporudi Yerusalemu nikawa naomba Hekaluni 18 nilim wona katika ndoto akiniambia ‘Harakisha uondoke Yerusalemu upesi kwa sababu watu hawa hawatakubali ushuhuda wako juu yangu.’ 19 Nikajibu, ‘Bwana, wanajua jinsi nilivyokuwa nikienda katika masinagogi nikawafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini wewe. 20 Na hata shahidi wako Stefano alipokuwa anauawa mimi nilikuwa nimesimama kando nikikubaliana na kitendo hicho na nikashika mavazi ya wale waliomwua. 21 Akaniambia, ‘Nenda, kwa maana nitakutuma mbali, kwa watu wa mataifa.”

22 Watu walimsikiliza Paulo mpaka hapo; kisha wakapaaza tena sauti zao wakasema, “Mwondosheni duniani! Mtu kama huyu hasta hili kuishi!” 23 Walipoendelea kupiga kelele na kupeperusha nguo zao na kutupa mavumbi juu hewani, 24 yule jemadari akaamuru wale askari wake wamwingize Paulo katika ngome na wamhoji na kum chapa viboko ili aeleze vizuri kwa nini wale Wayahudi walikuwa wanampigia makelele. 25 Lakini walipokwisha kumfunga kwa kamba za ngozi ili wamchape viboko, Paulo akamwambia askari aliyekuwa karibu naye, “Je, ni halali kumpiga raia wa Kirumi kabla hajahu kumiwa kwa kosa lo lote?” 26 Yule askari aliposikia maneno haya, alimwendea yule jemadari akamwuliza, “Unajua unalolifanya? Huyu mtu ni raia wa Kirumi.” 27 Kwa hiyo yule jemadari akaja akamwuliza Paulo, “Niambie, wewe ni raia wa Kirumi?” Paulo aka jibu, “Ndio.” 28 Yule jemadari akasema, “Mimi nilinunua uraia wangu kwa fedha nyingi.” Paulo akamjibu, ‘ ‘Lakini mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.” 29 Wale wote waliokuwa wamejiandaa kumhoji wakaondoka haraka haraka na yule jemadari akaingiwa na hofu, kwa maana alitambua ya kuwa alikuwa amemfunga raia wa Kirumi kinyume cha sheria.

Paulo Apelekwa Mbele Ya Baraza

30 Kesho yake yule jemadari alimfungua Paulo zile kamba ali zofungwa akaamuru makuhani wakuu na baraza lote likutane. Akamleta Paulo mbele yao ili apate kujua kwa nini Wayahudi wali kuwa wanamshtaki.

23 Paulo akawakazia macho wajumbe wa baraza, akasema, “Ndugu zangu, mimi nimeishi nikiwa na dhamiri safi kabisa siku zote mbele za Mungu, mpaka leo.” Kuhani mkuu Anania akaamuru wale waliokuwa karibu na Paulo wampige kofi mdomoni. Ndipo Paulo akasema, “Mungu atakupiga, wewe ukuta uliopakwa chokaa! Unawe zaje kusikiliza kesi hii kwa mujibu wa sheria, na hapo hapo, kinyume cha sheria, unaamuru nipigwe?” Wale watu waliokuwa wamesimama karibu wakamwambia Paulo, “Mbona unamtukana kuhani mkuu wa Mungu?” Paulo akajibu, “Ndugu zangu, sikujua kwamba yeye ni kuhani mkuu. Kwa maana Maandiko yanasema, ‘Usimseme vibaya kiongozi wa watu wako.’ ” Paulo alipotambua ya kuwa baadhi ya wajumbe wa baraza walikuwa Masadukayo na wengine ni Mafarisayo alisema nao kwa sauti kubwa, “Ndugu zangu! Mimi ni Mfarisayo, mtoto wa Mafarisayo; na hapa nimeshitakiwa kuhusu tumaini juu ya ufufuo wa wafu.” Aliposema haya, Mafarisayo na Masadukayo wakafarakana na baraza zima likagawanyika. Kwa maana Masadukayo wanaamini kwamba hakuna ufufuo, wala hakuna malaika au roho; lakini Mafarisayo wanaamini haya yote. Kelele zikazidi sana; na baadhi ya waandishi wa sheria wa upande wa Mafarisayo, wakasimama wakiwapinga wengine wakasema, “Hatuoni kosa lo lote alilofanya mtu huyu! Huenda ikawa malaika au roho amezungumza naye kweli!” 10 Mabishano yalipozidi kuwa makali, yule jemadari aliogopa kuwa wangeweza kumrarua Paulo vipande vipande. Kwa hiyo akaamuru askari wakamtoe Paulo alipokuwa, arudishwe kwenye ngome ya jeshi. 11 Usiku uliofuata, Bwana akamtokea Paulo akasimama karibu naye akamwambia, “Jipe moyo! Kama ulivyonishuhudia hapa Yerusalemu, itakubidi unishuhudie na huko Rumi pia.”

Njama Za Wayahudi Kumwua Paulo

12 Kulipopambazuka Wayahudi wakala njama ya kumwua Paulo. Wakaweka nadhiri kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamemwua Paulo. 13 Waliofanya mpango huu walikuwa zaidi ya watu arobaini. 14 Wakaenda kwa kuhani mkuu na wazee wakasema, “Tumeweka nad hiri ya pamoja kwamba hatutakula wala kunywa mpaka tumwue Paulo. 15 Kwa hiyo ninyi pamoja na baraza, pelekeni ombi kwa jemadari ili Paulo aletwe barazani, mtoe udhuru kwamba mnataka kuchunguza kesi yake kwa usahihi zaidi. Sisi tutakuwa tayari kumwua hata kabla hajakaribia kufika hapa.” 16 Basi kumbe binamu yake Paulo alisikia kuhusu mpango huu. Akaenda katika ngome ya jeshi akamweleza Paulo mambo haya. 17 Paulo akamwita mmoja wa wale maaskari akamwambia, “Mchukue kijana huyu kwa jemadari, ana neno la kumwambia.” 18 Yule askari akamchukua yule kijana mpaka kwa jemadari akamwambia, “Yule mfungwa Paulo aliniita akaniambia nimlete huyu kijana kwako, kwa sababu ana neno la kukuambia.” 19 Yule jemadari akamchukua yule kijana kando akamwuliza, “Unataka kuniambia nini?” 20 Naye akasema, “Wayahudi wameku baliana wakuombe kesho umpeleke Paulo kwenye Baraza lao kwa kisingizio kwamba wanataka kuchunguza kesi yake kwa uangalifu zaidi. 21 Lakini usikubali ombi lao kwa maana zaidi ya watu aro baini wamekula njama kwamba hawatakula wala kunywa mpaka wamwue Paulo nao wamejiweka tayari kumvizia ukishakubali ombi lao.” 22 Yule jemadari akamruhusu yule kijana aende, akamwonya akisema, “Usimwambie mtu ye yote kwamba umenieleza habari hizi.”

Paulo Apelekwa Kaisaria Kwa Gavana Feliksi

23 Yule jemadari akawaita maaskari wawili akawaambia, “Tay arisheni askari mia mbili watakaokwenda Kaisaria pamoja na askari wa farasi sabini, na askari wa mikuki mia mbili; nanyi muwe tay ari kuondoka leo saa tatu za usiku. 24 Pia tayarisheni na farasi watakaotumiwa na Paulo, mumpeleke salama mpaka kwa gavana Feliksi.” 25 Kisha akaandika barua kwa Feliksi kama ifuatavyo: 26 “Mimi Klaudio Lisia, nakuandikia wewe gavana mtukufu Feliksi. Salamu. 27 Mtu huyu alikamatwa na Wayahudi wakawa kar ibu kumwua, ndipo mimi nilipofika na askari wangu nikamwokoa kwa kuwa nilipata habari kwamba yeye ni raia wa Kirumi. 28 Nami nikampeleka mbele ya baraza lao ili nipate kujua kosa alilofanya. 29 Ndipo nikagundua ya kuwa alikuwa anashtakiwa kuhusu sheria yao, lakini hakuwa na kosa la kustahili kifo au kifungo. 30 Lakini nilipata habari kwamba kuna mpango wa kumwua nikaamua nimpeleke kwako mara moja, nikawaamuru washitaki wake walete mashtaka yao kwako.” 31 Basi wale askari wakamchukua Paulo usiku wakampeleka mpaka Antipatri kama walivyoamriwa. 32 Kesho yake wakarudi kituoni wakawaacha wale askari wa mikuki waendelee na safari pamoja na Paulo. 33 Walipofika Kaisaria walimpa Liwali ile barua na pia wakamkabidhi Paulo kwake. 34 Alipokwisha soma ile barua, alimwuliza Paulo ametoka jimbo gani. Alipofahamishwa kuwa anatoka Kilikia 35 alisema, “Nitasikiliza kesi yako mara tu washtaki wako watakapofika.” Akaamuru Paulo awekwe chini ya ulinzi katika ikulu ya Herode.

Mashtaka Ya Wayahudi Juu Ya Paulo

24 Baada ya siku tano, Kuhani Mkuu Anania akafika pamoja na baadhi ya wazee na wakili mmoja aitwaye Tertulo. Wakatoa mashtaka yao juu ya Paulo mbele ya Gavana. Na Paulo alipoitwa, Tertulo akaanza kutoa mashtaka akasema, “Mtukufu Feliksi, kutokana na uongozi wako wa busara tumekuwa na amani ya kudumu na tunatambua ya kuwa mabadiliko mengi muhimu yaliyotokea katika taifa letu yameletwa na uwezo wako wa kuona mbele. Wakati wote na kila mahali tunapokea mambo haya yote kwa shukrani za dhati. Lakini nisije nikakuchosha, nakuomba kwa hisani yako utusikilize kwa muda mfupi. Tumemwona mtu huyu kuwa ni mfanya fujo ambaye ana chochea maasi kati ya Wayahudi dunia nzima. Yeye ni kiongozi wa dhehebu la Wanazareti. Tena alijaribu kulichafua Hekalu letu lakini tulimkamata [tukataka kumhukumu kwa mujibu wa sheria zetu, lakini jemadari Lisia alikuja akamchukua kutoka kwetu kwa kutu mia nguvu akaamuru wanaomshtaki walete mashtaka yao mbele yako]. Wewe mwenyewe ukimwuliza maswali utathibitisha ukweli wa mashtaka yote tunayoleta mbele yako kumhusu yeye.” Wayahudi wakamwunga mkono wakithibitisha kwamba mashtaka yote yalikuwa ya kweli.

Paulo Ajitetea Mbele Ya Feliksi

10 Gavana Feliksi alipomruhusu Paulo ajitetee, yeye alisema, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi kwa hiyo natoa utetezi wangu bila wasi wasi. 11 Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipokwenda Yerusalemu kuabudu. 12 Hawa wanaonish taki hawakunikuta nikibishana na mtu ye yote au nikianzisha fujo katika Hekalu au katika sinagogi au mahali pengine po pote mjini. 13 Wala hawawezi kabisa kuthibitisha mambo haya wanayon ishtaki. 14 Lakini nakiri mbele yako kuwa mimi namwabudu Mungu wa baba zetu kwa kufuata ile ‘Njia’ ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kilichoandikwa katika Sheria ya Musa na Mana bii 15 na ninalo tumaini kwa Mungu ambalo hata na wao wanaliku bali, kwamba kutakuwa na ufufuo wa wote, walio na haki na wasio na haki. 16 Kwa hiyo ninafanya kila jitihada kuishi nikiwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu. 17 Basi, baada ya kuwa nje ya Yerusalemu kwa miaka kadhaa nilikuja mjini kuwale tea watu wa taifa langu sadaka kwa ajili ya maskini na kutoa dha bihu. 18 Nilikuwa nimeshatakaswa waliponikuta Hekaluni nikifanya mambo haya, na hapakuwa na umati wa watu wala fujo yo yote. 19 Lakini kulikuwa na Wayahudi kutoka Asia, nadhani nao walista hili wawepo hapa mbele yako ili watoe mashtaka yao kama wanalo lo lote la kunishtaki. 20 La sivyo, watu hawa waseme ni kosa gani walilogundua nimefanya niliposhtakiwa mbele ya Baraza, 21 isipo kuwa lile jambo nililotangaza wazi wazi nilipojitetea mbele yao, kwamba, ‘Mimi nimeshtakiwa mbele yenu leo kuhusu ufufuo wa wafu.’

22 Ndipo Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia, akaamua kuahirishwa kwa kesi, akasema, “Mara jemadari Lisia atakapofika nitatoa hukumu yangu juu ya kesi hii.”